Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Dk Oscar Kikoyo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es salaam jana juu ya hali ya usafiri kipindi cha siku kuu za Krismas na mwaka mpya ambapo ametahadharishja abiria kuto kukubali kutozwa nauri za juu na pindi ikitokea hivyo Sumatra ipewe taarifa haraka.
BARAZA
la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini
(SUMATRA Limewakumbusha wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani na
Madereva kufuata Masharti ya Leseni zao kwa kutotoza nauli kubwa
katika kipindi hiki cha Sikuku za mwezi Desemba na endapo mtu akikiuka
sheria basi Mamlaka hiyo haitosita kumfutia Leseni ya Basi
litakalokwenda kinyume.
Hayo
yamesemwa Mda huu Jijini Dar Es Salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza la
Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini
(SUMATRA) Dk Oscar Kikoyo Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari
ambapo,
Dk
Kikoyo alisema kutokana na wingi wa abiria na mahitaji ya usafiri kuwa
makubwa katika kipindi hiki cha sikuku na kupelekea mahitaji zaidi ya
usafiri ,baadhi ya watoa huduma wamekuwa wakichukulia kipindi hiki kama
njia ya kuvuna zaidi kutoka kwa watumiaji kwa kuongeza nauli maradufu.
Dk
Kikoyo aliongeza kuwa Baraza hilo linatoa wito kwa Wamiliki wote wa
mabasi kuwahimiza wafanyakazi na mawakala wao wanaokata tiketi katika
vituo mbalimbali nchini kuwa waaminifu kwa waajiri wao na wateja wao.
Vilevile
Dk Kikoyo alisema baraza hilo likatoa wito pia kwa watu wote hasa
Abaria wanaotarajiwa kusafiri kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kufanya
maandalizi ya safari zao mapema ili kuepuka matatizo ya kulanguliwa
tiketi na kupewa risiti tiketi watakazokata.
Aidha,Dk Kikoyo alisema kuwa endapo abiria yeyote ambaye atatozwa
nauli zaidi na kukataliwa kufanya Bookings zao mapema basi asisite
kutoa taarifa kwenye Mamlaka husika kwa namba ya simu 022 2127410,0787787621,0800110019 au 0800110020 ili Dereva wa Basi hilo pamoja na Mmiliki wake wachukuliwe hatua.
|
Thursday, December 4, 2014
KUELEKEA SIKUKUU HIINDIO KAULI YA SUMATRA JUU YA USAFIRI WA MIKOANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment