Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kimeingia kambini leo (Desemba 1
mwaka huu) Bulyanhulu mkoani Shinyanga kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya
Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ikiwa chini ya Kocha Mart Nooij, Stars Maboresho itapiga kambi
mkoani humo hadi Desemba 6 mwaka huu ambapo itarejea jijini Dar es Salaam
tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa.
Wachezaji walioingia kambini ni Abubakar Ally (Coastal Union), Abubakar
Ally Mohamed (White Bird), Aishi Manula (Azam), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Atupele
Green (Kagera Sugar), Edward Charles (Yanga) na Emmanuel Semwanda (African
Lyon).
Gadiel Michael (Azam), Hashim Magoma (Stand United), Hassan Banda
(Simba), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Joram Mgeveke (Simba), Kassim Mohamed
Simbaulanga (African Lyon), Kelvin Friday (Azam) na Makarani Ally (Mtibwa
Sugar).
Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Muzamir Ally (Mtibwa
Sugar), Omari Nyenje (Ndanda), Pato Ngonyani (Yanga), Rashid Mandawa (Kagera
Sugar), Said Hamisi (Simba), Salim Hassan Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shiza
Ramadhan (Mtibwa Sugar).
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaishukuru kampuni
ya kuchimba madini ya Acacia Mining PLC (zamani African Barrick Gold PLC) kwa
kufadhili kambi ya Stars kupitia mgodi wa Bulyanhulu.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment