Michuano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake ya Proin
Women Taifa Cup inaanza rasmi Desemba 28 mwaka huu kwa mechi ya ufunguzi kati
ya timu za mikoa ya Mara na Mwanza itakayochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza.
Kombaini
za mpira wa miguu za mikoa yote ya Tanzania Bara zitashiriki mashindano hayo
yatakayochezwa kwa raundi mbili mwanzoni, na baadaye hatua ya robo fainali hadi
fainali.
Mashindano
hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin Promotions Limited, kuanzia hatua ya robo
fainali, mechi zote zitafanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja
Biashara wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Peter Simon Shankunkuli aliishukuru
kampuni ya Proin ambao ni watengenezaji, wazalishaji na wasambazaji wa filamu
za kitanzania kwa kuwezesha mashindano hayo kufanyika kwa mara ya kwanza.
Proin
Promotions imekua ikivumbua vipaji mbalimbali vya uigizaji na sasa imeamua
kujikita katika mpira wa miguu ili kuweza kuvumbua vipaji kwa wachezaji wa kike.
Shankunkuli
alisema nafasi bado zipo kwa wadhamini watakaoguswa na mashindano hayo, kwa
kuwasiliana na TFF au Proin Promotions Limited kwa maelezo zaidi.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
|
No comments:
Post a Comment