Kampuni ya Global Education Link (GEL) kwa kushirikiana na Ofisi ya
Waziri Mkuu (TAMISEMI), Wizara ya Elimu na Ufundi pamoja na Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) wameandaa maonyesho ya kwanza
ya kimataifa ya elimu (TIEE) yanayotarajiwa kufanyika Disemba 17 hadi
21 mwaka huu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Global link
Education, Abdulmalik Mollel, alisema lengo la maonyesho hayo ni
kutambulisha wadau wa elimu kwa pamoja ili kuweza kutoa huduma ya pamoja
kwa wananchi na kuwaelimisha juu ya mambo muhimu yaliyopo katika kila
sekta.Alisema ushiriki wa asasi mbalimbali kwa kushirikiana na sekta binafsi
utakuwa na chachu ya mabadiliko ya elimu kwa kupitia mpango wa matokeo
makubwa sasa.Maonesho hayo yanatarajiwa kupata washiriki zaidi ya 500 na wananchi mbalimbali zaidi ya 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment