Baadhi ya wanahabari wakiwa kazini kurekodi mkutano wa
menejimenti ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) jijini Dar es Salaam leo walipokuwa wakitoa ufafanuzi
juu ya tatizo lililojitokeza jana Desemba 3, 2014 ambapo wateja wa benki hiyo
walishindwa kutumia huduma za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi
(Mobile Banking).
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Uongozi wa NBC umebaini kuwepo kwa ujumbe kupitia
mitandao ya jamii unayohusisha NBC na wizi wa fedha za wateja kwa kupita
mashine za kutolea fedha (ATM). Ujumbe huo huo unahamasisha
wateja kutoa fedha kwenye akaunti zao.
NBC tunapenda kuwafahamisha wateja wetu na umma kwa
ujumla kwamba ujumbe huo hauna ukweli wowote. Papo hapo, matukio ya miamala ya
wizi ni tatizo ambalo linaendelea kutafutiwa utatuzi na mabenki yote yaliyo
chini ya Chama cha Mabenki Tanzania (TBA).
Tunapenda kuwahakishia wateja wetu na umma kwamba NBC
inaendelea kudhamiria kuwapatia wateja wetu huduma bora na ya kisasa.
Imetolewa na uongozi
|
No comments:
Post a Comment