Alliance
for Change and Transparency
(ACT-Tanzania)
___________________________
________
Maazimio
ya Halmashauri Kuu ya ACT-Tanzania kufuatia Mkutano wake wa Pili
Uliofanyika Jumatatu Tarehe 12 Januari
2015 katika Hoteli ya Kagame, Jijini Dar es Salaam
Halmashauri
Kuu ya ACT-Tanzania ilifanya Mkutano wake wa Pili wa kawaida siku ya Jumatatu
tarehe 12 Januari 2015 katika Hoteli ya Kagame Jijini Dar es Salaam. Pamoja na
mambo mengine, Halmashauri Kuu ilipokea na kujadili taarifa mbalimbali na kutoa
maamuzi na maazimio katika mambo mbalimbali kama ifuatavyo:
1.
Halmashauri Kuu ilipokea,
kujadili na KUPITISHA k Mwongozo na Kanuni za Uchaguzi ndani ya Chama cha
ACT-Tanzania. Halmashauri Kuu imepanga uchaguzi ndani ya chama ufanyike kuanzia
tarehe 17 Januari 2015 katika ngazi
ya Shina na kukamilika tarehe 28 Machi
2015 katika
ngazi ya Taifa.
Kadawi limbu |
2.
Halmashauri Kuu ilipokea na
kujadili Taarifa ya Kamati Maalumu ya Nidhamu iliyoundwa na Kamati Kuu
kuchunguza masuala ya nidhamu ya viongozi wa Kitaifa, ambao ni Mwenyekiti wa
Muda wa Taifa Ndugu Kadawi Lucas Limbu na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Leopold
Mahona. Baada ya mjadala wa kina na kuridhishwa na makosa yaliyotendwa na viongozi
hawa, Halmashauri Kuu imetoa maamuzi yafuatayo:
a.
Imemsimamisha Ndugu Kadawi
Lucas Limbu katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Muda wa Taifa baada ya kupigiwa
kura ya kutokuwa na imani na wajumbe 57 (87.7%) kati ya wajumbe 65
waliohudhuriwa.
b.
Imemwondoa katika nafasi yake
ya Naibu Katibu Mkuu Ndugu Leopold Mahona baada ya wajumbe 57 (87.7%) kupiga
kura za kuunga mkono pendekezo hilo kati ya wajumbe 65 waliohudhuria.
3.
Halmashauri Kuu imeazimia
kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na imeagiza Kamati Kuu
kujiandaa na uchaguzi huo katika ngazi zote.
Pamoja
na salamu za uzalendo za ACT-Tanzania
Samson
Mwigamba
No comments:
Post a Comment