Tigo imetangaza
leo kwamba Meneja Mwendeshaji wa kampuni hiyo, Diego Gutierrez, atang’atuka
kutoka katika nafasi yake Aprili 1 mwaka huu kwa ajili ya majukumu mengine
aliyopewa katika kampuni mama ya Tigo kimataifa, Millicom. Nafasi yake
itakayoachwa wazi itachukuliwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa muda Bi. Cecile
Tiano atakaye anza kazi nchini wiki hii.
Bw. Gutierrez
amepata mafanikio makubwa kuongoza kampuni ya Tigo Tanzania akitokea Ghana
mwaka 2009. Alijiunga na Tigo Tanzania kwanza kama Naibu Meneja Mwendeshaji na
baadaye akapandishwa cheo kuwa Meneja Mwendeshaji kamili kuanzia mwaka 2012
hadi sasa, na siku zote amekuwa kiungo muhimu katika kuleta maendeleo ya
Tigo.
Katika muda wake, kampuni imekuwa kwa zaidi ya asilimia 100% kufikia
idadi ya wateja milioni 8, pia imesambaza huduma ya kasi ya mtandao 3G,
pamoja na huduma ya kutuma na kupokea fedha, vilevile imekuwa kampuni
inayoongoza kwa ubunifu kwa kuleta huduma na bidhaa mbali mbali kama Facebook
ya bure, wateja kupewa gawio kupitia Tigo Pesa, utumaji na upokeaji wa fedha
kwa urahisi zaidi kati ya Tigo na makampuni mengine ya simu, pamoja na huduma
ya kutuma na kupokea fedha kati ya Tanzania na nchi za jirani iliyo na uwezo wa
kubadilisha ankara ya fedha moja kwa moja.
Kwa utaalamu
huo katika huduma ya kutuma na kupokea fedha, Bw. Gutierrez
anapandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Huduma za Kutuma na Kupokea Fedha kwa bara la
Latin Amerika.
Bi. Cecile
Tiano anajiunga na menejimenti ya Tanzania akitokea kuwa Kaimu Meneja
Muendeshaji wa Tigo nchini DR Congo. Kabla ya hapo alikuwa mshauri wa kitalaam
kwa kampuni za Tigo Ghana na Tanzania akiwa na uzoefu wa kufanya kazi
kama afisa mwandamizi katika sekta za mawasiliano, habari na intanet.
Akizungumzia
kuhusu mabadiliko haya, Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Millicom kwa bara la
Africa Bw. Arthur Bastings alisema kwamba, “Diego amefanya kazi nzuri sana
Tigo, ameweza kuleta ubunifu wa kipekee katika soko hili na kuanzisha huduma
nyingi sana ambazo zimekuwa za kwanza kuzinduliwa duniani kutoka Tigo
Tanzania. Kwa nafasi kubwa jitihada zake zimefanya Tanzania kuwa
kinara duniani katika sekta ya Huduma na Kupokea fedha kwa njia
ya simu na pia intanet imekuwa ya gharama nafuu kwa idadi kubwa ya
watu nchini Tanzania.
Tunamtakia kila la kheri katika nafasi yake mpya huku
tukimkaribisha pia Cecile nchini Tanzania. Cecile ni afisa mwandamizi katika
sekta ya biashara aliyeweza kupata mafanikio makubwa katika uzoefu wake wa kazi
na nina imani kubwa kwamba ataendelea kuwapatia uongozi mzuri menejimenti ya
Tigo Tanzania.”
No comments:
Post a Comment