BW ;JULIUS MTATIRO KADA WA CHAMA CHA CUF
SOMA KAULI YAKE HAPA
RAIS KIKWETE ANASEMA KUANZIA MWAKA 2016 CCM ITATOA ELIMU YA SEKONDARI BURE...
Kwa
nini aanze kupanga sera za serikali ijayo wakati yeye atakuwa Msoga,
kijijini kwake? Na kama yeye ni bingwa wa mipango mbona mwaka huu peke
yake vijana zaidi ya 20,000 wamerudi majumbani kwao kwa sababu wamekosa
mkopo wa elimu ya juu? Wakati
Rais anasema hayo nimejionea jana wafanyakazi wa TAZARA wakianza mgomo
kwa sababu hawajalipwa mishahara ya miezi mitano, wakati huohuo nimeona
walimu Kinondoni wakiandamana kudai fedha zao. Badala
ya kuanza kufikiri kipropaganda dhana ya kusomesha sekondari bure mwaka
kesho, kwa nini tusilipe ada za watoto hawa masikini wa vyuo vikuu
ambao wanahitaji msaada sasa hivi ili hayo ya mwaka kesho tuyapange
wakati wa kampeni mwezi oktoba 2015? Vyama vya upinzani viliposema
utoaji wa elimu bure mwaka 2000, 2005 na 2010, CCM ilisema vinaongopa na
haiwezekani na wananchi waliamini uongo wa CCM. Hata hiyo elimu ya
msingi tu CCM imeshindwa kutoa bure, michango iliyopo sasa inazidi ada
ya zamani. Kinachoonekana hapo ni propaganda za kuanza kuwaweka sawa
wananchi kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka. Si ajabu kuwa, Kinana na
Nape watazunguka nchi nzima katika mikutano yao ya mwaka huu, wakieleza
sera hii ya elimu ya sekondari ambayo kuitekeleza hawawezi. Na hapohapo wanasahau kuwa mambo mengi yaliyoahidiwa na CCM mwaka 2010 hayajatekelezwa, Mahakama ya kadhi siioni, waliahidi! Ni
jambo la ajabu mno kukuta kiongozi wa nchi ambaye anamaliza muda wake
anaanza kupanga ahadi za serikali ijayo, wakati uongozi wake umeacha
majanga mengi katika nchi huku ukishindwa kutekeleza ahadi zake nyingi!
Sijui mnanielewa? J. Mtatiro, Dar Es Salaam, 11 Januari 2015 |
No comments:
Post a Comment