Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, SHEKH RAJAB KATIMBA akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam. |
NA KAROLI VINSENT
JUMUIYA na Taasisi za Kiislam Nchini imesema itawahamasishwa Waumini wa
Kiislam popote walipo nchini kuipigia kura ya Hapana katiba iliyopendekezwa na
Bunge maalum la Katiba, pamoja na kuukataa Mswaada wa Marekebisho ya sheria
mbalimbali wa namba 2 wa mwaka 2014 unaotarajiwa kuwasilishwa kwenye Bunge
lijalo kutokana na Serikali kuwadanganya waislam nchini.
Kutokana na kitendo chake Serikali kupuuza matakwa yao wanaodai uwepo wa
Mahakama ya Kadhi ambao wanasema ilikuwepo kwenye makubaliano kati ya Serikali
na Waislam nchini juu ya uwepo wa Mahakama hiyo.
Wanahabari mbalimbali wakisikiliza kwa makini |
Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislam nchini, Rajabu Katimba wakati wa Mkutano na Waandishi wa
Habari ambapo alisema waislam wamechoka na ubabaishaji unaofanywa na
serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kulitekeleza Azimio la uundwaji wa
Mahakama ya Kadhi nchini.
“Kwani
hata mswaada wa marekebisho ya kisheria mbalimbali unaowasilishwa na serikali
hautakuwa na tija kwa waislam nchini na umekuwa na propaganda nyingi za
unzishwaji wa mahakama ya kadhi lakini hauna utekerezaji na ndio sababu
tunasema hakuna nia ya dhati kati ya serikali ya CCM na Waislam”
“Nchini kwani wametudanganya
kwenye Ilani yao ya Mwaka 2005 ilituhaidi kuanzisha mahakama ya kadhi lakini
kwa ghilba nyingi CCM haikutekeleza ahadi hiyo baada ya kuingia madarakani kwa
hoja kuwa hili ni Jambo la Kikatiba”alisema katimba
SHEKHE Katimba alizidi kusema kwa Uchungu kwamba
“hata wakati wa Bunge la katiba lilokuwa limeundwa na wajumbe wengi wa
CCM hawakuona umuhimu wa kutimzi ahadi yao ya kuweka Mahakama ya Kadhi
katika katiba pendekezwa na kwani wajumbe wengi wa CCM walishangilia Jambo hili
ili hali wanajua Dhahiri kuwa Waislamu hawakufurahishwa na uamuzi wao na pia
walikiuka ilani yao na ahadi kwa Waislam”
Aidha,Shekhe Katimba alisema hata mswaada ambao wanaukataa wa merekebisho ya
Sheria wa namba 2 wa mwaka 2014 unakasoro nyingi ambazo wanasema hauna tija kwa
waislam katika kipengere cha Mahakama ya Kadhi-
Ikiwemo Mswaada umempa
mamlaka “MUFTI”kuteua makadhi na kuengeneza kanuzi za Uendeshaji wa mahakama ya
Kadhi ili hali sio chombo cha Sheria,na pia Mswaada huo umempa Mufti-
Mamlaka ya kutenganisha kanuni za uendeshaji wa mahakama za kadhi ambalo
wanasema ni jambo la ajabu kwani ofisi ambayo haiundwi na sheria na mamlaka ya
kuengeneza kanuni za chombo.
Shekhe Katimba
alisema hata Mswaada wa kuikataa ,mahakama ya kadhi ijiendeshe yenyewe badala
ya kuendeshwa na Serikali ni Jambo ambalo haijawahi kutokea Sehemu yeyote
duniani Chombo, kama mahakama kujiendesha yenyewe.
Hata Hivyo Shekhe Katimba
aliwataka waislam kwa Ujumla kutoipigia kura ya Ndio wakati wa kupigia kura
katiba iliyopendekwa na Bunge mwezi March mwaka huu kwakuwa katiba hiyo haina
nia nzuri kwa Waislam nchini
No comments:
Post a Comment