Naibu katibu mkuu wa CUF bi MAGDALENA SAKAYA akizungumza na wanahabari mapema leo makao makuu ya chama hicho juu ya uapishwaji wa viongozi wa serikali za mitaa unaoendelea nchini |
Chama cha wananchi CUF kimetangaza kulaani vikali
zile wanazoziita vurugu na hujuma
wanazodai zinafanywa na chama cha
mapinduzi CCM katika zoezi la uapishwaji wa viongozi wa serikali za mitaa
linaloendelea nchi nzima.
Akizugumza na wanahabari mapema leo Naibu katibu
mkuu wa chama hicho bi MAGDALENA SAKAYA amesema kuwa mkakati wa ccm ulianza
katika zoezi la uchaguzi huo katika kubatilisha matokeo ambayo chama cha CUF kilishinda
na sasa CCM imeamua kutumia mbinu chafu ya kutaka kuwaapisha viongozi wao ambao
hawakushinda katika matokeo ya uchaguzi huo.
Wanahabari mbalimbali wakisikiliza kwa makini |
Akitaja maeneo kadhaa ambayo wagombea wa CUF
walishinda lakini wasimamizi wa uchaguzi wakashindwa kuwatangaza na badala yake
kuwapeleka viongozi wa CCM kwenda kuapa kuwa ni mtaa wa mwinyimkuu kata ya
mzimuni kinondoni ambapo mgombea wa cuf HASSAN ABUBAKARY alishinda katika
uchaguzi huo lakini msimamizi wa uchaguzi huo aliitisha uchaguzi mwingine
uchaguzi ambao uligomewa na wanachi na badala yake akatangazwa mgombea wa CCM,
FUNUA ALLY kuwa ndiye mshindi.
Mtaa mwingine ni mtaa wa ukwamani kata ya kawe ambapo
mgombea wa cuf alishinda lakini fomu za ushindi hazikusainiwa hadi leo na
badala yake mgombea wa ccm ndiye ametangazwa mshindi. Aidha maeneo mengine
ambayo amesema yamefanyika mchezo huo ni mtaa wa msisiri kata ya
mwananyamala,mtaa wa kiwalani kata ya migombani,mtaa wa kigogo fresh,pamoja na
mtaa wa malapa,kinyerezi,migombani,bunda mara,pamoja na maeneo mengine ambayo
wanachi wanazidi kurepoti tukio hilo.
Aidha bi SAKAYA amesema kuwa kutokana na
uchakachuaji huo mkubwa ni wazi kuwa lazima viongozi waliohusika ikiwa ni
pamoja na mkurugenzi wa uchaguzi wa kinondoni na waziri husika wawajibike kwa
kuachia nafasi zao mara moja kwani ni aibu kwa taifa kuwaibia wanachi kwa kiasi
hicho.
Aidha amekionya chama cha mapinduzi kwa kile
alichosema hii ni mipango yao ya kuiviuruga Amani ya Tanzania kuwa nguvu ya
umma waliyokutana nayo uchaguzi huu itakuwa ni Zaidi katika uchaguzi ujao hivyo
mbinu chafu hazitavumilika hata mara moja.
Kumeshughudiawa vihoja katika zoezi la kuapishwa
viongozi wa serikali zaa mitaa jijini Dar es salaam ambapo katika ukumbi wa
landmari pamoja na kule ilala juzi
kulizuka fujo kubwa baada ya kugundulika kuwa kuna viongozi ambao hawakushinda
ila walipewa barua za kwenda kuapishwa jambo ambalo wanachi hawakuliafiki na
kusababisha fujo kubwa.
No comments:
Post a Comment