Kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bi SOPHIA MJEMA akimkabidhi cheti mmoja wa maofisa wa jeshi hio waliopewa zawadi kwa azi yao kubwa wanayolifanyia jeshi hilo |
Watanzania ambao wanamiliki silaha nchini bila
kibali maalum wametakia kuzisalimisha ndani ya jeshi la polisi mara moja kwani
umiliki wa silaha hizo ni kinyume na sheria za Tanzania na endapo utakutwa na
silaha hio sheria itachukua mkondo wake.
Wito huo umetolewa leo na kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bi SOPHIA MJEMA katika sherehe za utoaji wa zawadi kwa maofisa wakaguzi na askari wa Vyeo mbalimbali wa jeshi la polisi shughuli iliyofanyika katika chuo cha Taaluma ya polisi jijini Dar es salaam ambazo zimetolewa na kamishna wa polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam SULEMAN KOVA.
Akizungumza katika shughuli hiyo kaimu muu wa mkoa
wa Dar es salaam Bi SOPHIA MJEMA amesema kuwa hali ya amani katika jiji la Dar es salaam na
nchini kwa ujumla itakuwepo endapo wanachi watatii sheria bila shuruti ikiwa ni
pamoja na kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua wahalifu hasa wale ambao
wanakuwa na silaha za kufanyia uhalifu kinyume na sheria.
Bi SOPHIA amelipogeza jeshi la polisi kwa kuendelea
kupambana na uhalifu huo ambapo wamefanikiwa kukamata silaha mbalimbali za
kufanyia uhalifu ambapo amewataka kuongeza kasi katika zoezi hilo ili
kuhakikisha ulalifu katia jiji la Dar es salaam unakuwa ni jambo la historia
tu.
Aidha akizungumzia swala la baadhi ya wanachi
wanaokuwa wanatembea na pesa nyingi kwa pamoja katika mifuko amesema kuwa
mtindo huo ni mtindo wa kizamani na
unashawishi uhalifu kwani kwa sasa kuna njia nyingi za kisasa za kusafirisha
pesa bila kubebe mabulungutu ya hela ambayo mara nyingi.
Katika zoezi hilo jumla ya maofisa wakaguzi na
askari 107 kutoka kinondoni,ilala na temeke wamepewa zawadi na jeshi hilo kwa
kazi nzuri wanayolifanyia jeshi hilo.
ENDELEA KUFWATILIA TUKIO NZIMA HAPO CHINI
Wadau wa B-PESA wakiwa katika dhughuli hiyo ambayo nao ni wadau wa kusafirisha pesa kwa njia salama |
Maofisa wa polisi ambao leo wamepewa zawadi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya zoezi nzima |
Kaimu muu wa mkoa wa Dar es salaam Bi SOPHIA MJEMA akizungumza katika hafla hiyo |
No comments:
Post a Comment