Katibu mkuu wa Taasisi za kiislam Tanzania shekh KHAMIS MATAKA akisoma hotuba yeke wakati akifungua kongamano hilo leo Jijini Dar es salaam. |
NA EXAUD MTEI
Waumuni
wa dini ya kiislam na dini nyingine nchini Tanzania wametakiwa kuahikikisha
kuwa hawaruhusu aina yoyote ya chuki za kidini ambazo zitapelekea kutokuelewana
na kuleta machafuko hususani kipindi hiki ambacho Tanzania iko katika mambo muhimu
ya uchaguzi mkuu.
Wito
huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam katika kongamano la kidini la siku mbili
lililoandaliwa na taasisi ya kiislam ya IMAM BUKHARY ISLAMIC FOUNDATION kongamano
ambalo linawahusisha viongozi mbalimbali wa dini tofauti nchini Tanzania.
Akifungua
kongamano hilo leo mgeni rasmi ambaye ni katibu mkuu wa tasisi za kiislam Tanzania
shekh KHAMIS MATAKA amesema kuwa tofauti za kidini baina ya watanzania sio
chanzo cha kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani bali ni moja ya njia ya
kuwaunganisha watanzania na kuwafanya wawe kitu kimoja.
Amesema kuwa
machafuko mengi ambayo huwa yanatokea katika nchi mbalimbali duniani husababishwa
na chuki za kidini ambazo hupandikizwa na mataifa makubwa kwa lengo na
kuwagombanisha ili wao waweze kuingia kwa urais jambo ambalo amesema kuwa ni la
kupiga marufuku mara moja .
Askofu FILBERT MBEPELA ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa dini za kikiristo waliohudhuria kongamanno hilo akizungumza. |
Aidha amesema kuwa kuelekea kipindi hiki cha
uchaguzi sio kipindi cha viongozi wa dini kujiingiza katika siasa kwa kuwapigia
debe baadhi ya wagombea bali ni kipindi cha viongozi wa dini kukaa pamoja na
kutumia dini zao kuliombea taifa na kuacha mambo ya siasa kuendeshwa na
wanasiasa wenyewe tofauti na sasa ambapo kumeonekana wazi kuwa kuna muingiliano
wa viongozi wa dini kuingia katika maswala ya siasa.
Aidha akizungumza kwa niaba ya viongozi wa kikristo
waliohudhuria kongamano hilo askofu FILBERT MBEPELA amesema kuwa huu ni muda wa
dini zote nchini kuungana kwa pamoja kulitetea taifa la Tanzania na kuepuka
chuki na fitna ambazo mwisho wake zitaleta madhara makubwa kwa taifa yakiwemo
mauaji yasiyo ya haki.
Hizi ni baadhi ya piocha ambazo zinaonyesha madhara ya chuki za kidini ambazo mwishowe huzalisha vutrigu na mauaji makubwa katika mataifa mbalimbali |
Kongamano hilo litafanyika siku mbili ambapo lengo
kuu ni kuwakutanisha viongozi wa kiislam
na baadhi ya viongozi wa dini nyingine mbali
mbali kujadili hali ya amani duniani na kuona jinsi kgani Tanzania inaweza
kuepuka machafuko ya kidni kama yawayowakuta mataifa mengine kama Iraq,Libya,Syria
na nchi nyingine za kimagharibi.
No comments:
Post a Comment