Kituo kinachomilikiwa na shirika la Umeme nchini Tanesco picha na maktaba picha kamili itakujia |
NA KAROLI
VINSENT
WATU
wasiojulikana wamekivamia kituo cha upozaji na usambazaji wa umeme
nchini TANESCO kilichopo Uwanja wa ndege Jijini Dar es Salaam na
kuiba waya wenye Thamani ya Milioni 150 za kitanzania na kutokomea
kusiko
julikana
Na kulifanya Shirika la Umeme
nchini kukwama kuwasha Jenereta za kituo hicho ambacho walitarajia kuwanya
mwezi marchi mwaka huu.
Akithibitisha kutokea kwa wizi huo leo Jijini Dar es Salaam Meneja wa ugawaji na usambazaji wa
Umeme wa shirika hilo bwana Emmanueli Maniraboma Wakati alipotembelewa
na vyombo mbalimbali vya Habari,ambapo alisema wizi huo wa waya
umekwamisha mipango ya kuwasha mitambo mbalimbali ya umeme kituoni hapo.
“Kutokana na
wizi huu tumekwama kufanya mambo mengi yenye maendeleo katika kituo
hiki,kwani tulitarajia kuwasha mitambo hii ili watumiaji wa umeme
watumia vizuri na kutokana wizi huu,sasa tumekwama kabisa”alisema Bwana
Maniraboma.
Bwana
Maniraboma
aliongeza kuwa waya hizo zilizoibia hazipatikani nchini na mpaka
kuzileta nchini ilitumia zaidi ya milioni 150
za kitanzania kwa kutumia usafiri wa meli na wakitumia usafiri wa
ndege gharama zitaongezeka na kufikia fedha za kitanzania zaidi ya
milioni
200.ambapo uagizaji wake utachukua zaidi ya miezi mitatu.
Aidha,bwana
Maniraboma alisema kutokana na wizi huo shirika limechukua hatua ikiwemo
kufanyia uchunguzi juu ya hujuma wizi huo na ikibainika hatua kali za kisheria
zichukuliwe kwa walinzi wanaorinda kituo hicho.
Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa sheria na Uchunguzi wa Shirika la Umeme TANESCO lenin Kiabya alisema kwa sasa wako kwenye uchunguzi ikiwemo kwa walinzi wanaorinda kituoni hapo na ikibainika kama wao walizembea mpaka wizi huo kutokea watachukuliwa hatua kali za kisheria
No comments:
Post a Comment