Mwenyekiti wa profesa CUF IBRAHIM LIPUMBA akiwasili katika mkutano huo na wanahabari muda mfupi uliopita |
Kwa mara ya Kwanza tangu kutokea kwa vurugu za
kisiasa ambazo zilisababisha mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF profesa
IBRAHIM LIPUMBA kupigwa na kukamatwa na jeshi la polisi na hatimaye kupelekwa
mahakamani mwenyekiti huyo amejitokeza leo jumapili mbele ya wanahabari na
kueleza hali halisi ya tukio hilo huku akieleza adhma yake ya kutaka kumuona rais
kikwete kumueleza matatizo ambayo polisi wa Tanzania wanayo ambayo yanapaswa
kuzibitiwa mara moja.
Akizungumza kwa uchungu mkubwa LIPUMBA amesema kuwa
kilichotokea juzi huko mbagala ni ishara tosha kuwa Tanzania hakuna amani na
democrasia ya kweli kwani kuzuia maandamanao ambayo kila mwaka huwa yanafanyika
kwa amani na utulivu ni kuwanyima haki watanzania ya kuwakumbuka ndugu zao
waliofariki katika vurugu za Zanzibar.
Amesema kuwa kitendo walichokifanya polisi
kimewasikitisha sana wao kama wapenda amani na haki kwani polisi hao walikuwa
na taarifa tangu tarehe 22 mwezi wa kwanza ila wao wakaja kupiga marufuku
maandamano hayo terehe 26 jioni jambo ambalo ni kinyume na utaratibu kwani
hawakuwa na muda wa kuwaambia wanachama wao kuwa maandamano hayo yamepigwa
marufuku.
“sasa nafanya utaratibu wa kistaarabu kabisa wa
kwenda kuonana na rais kikwete na lengo langu ni moja tu la kutaka kumueleza
uhalisia wa jeshi la polisi na vitendo vibaya wanavyovifanya kwani tukiendelea
kufumbia macho matukio kama haya mwisho wa siku tutajikuta mahali pabaya sana
sisi kama nchi hivyo nataka kumueleza kuwa tusiruhusu hali hiyo itokee.”amesema
lipumba.
Aidha akizungumzia kauli ya serikali iliyotolewa
bungeni na waziri wa mambo ya ndani mh MATHIAS CHIKAWE kuwa CUF walikaidi
maagizo ya polisi ya kusitisha maandamano na ilikuwa ni njia ya kujitafutia
umaarufu wa kisiasa amesema kuwa ni kauli za kutunga na uzushi mkubwa na kauli
hizo zimeonyesha ni jinsi gani serikali imedhamiria kuwapiga wananchi kisawa
sawa katika matukio kama hayo.
Mnamo tarehe 27 mwezi wa kwanza CUF walikuwa wafanye
maandanano ya amani kuwakumbuka wanachama wenzao waliouawa huko zanzibari
lakini maandamano hayo yaliishia mikononi mwa jeshi la polisi huko mbagala.
Aidha amewashukuru sana watanzania hususani vyombo vya habari kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa katika sakata hilo na kuuweka ukweli wa jambo hilo wazi ambapo kila mtanzania ameweza kufahamu ni nini kimetokea.
No comments:
Post a Comment