Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC
kinashiriki kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ambayo yanafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dare s salaam na
kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa utoaji haki nchini ambapo LHRC ni moja kati
ya wadau hao.
Katika maadhimisho hayo ambayo yamezindiliwa leo na
rais mstaafu wa awamu ya pili mzee ALLY HASSAN MWINYI yemeenda sambamba na
uzinduzi wa report mbili za LHRC zinazoonyesha mwenendo wa kesi ambazo kituo
hicho kinapokea na kesi za ardhi ambazo zinarepotiwa katika kituo hicho.
Akizungmza na mtandao huu katika banda la kituo hicho
ndani ya viwanja vya mnazi mmoja afisa program dawati la ufwatiliaji na
utendaji wa mahakama Bi ROSEMARY MANASE amesema kuwa kituo hicho kimezindua report
mbili ambayo moja inaonyesha aina ya kesi ambazo zimeripotiwa kwao na ambazo wameshughulika nazo report ambayo
amesema kuwa wataisambaza kwa wadau wote kwa lengo la kuwasaidia katika
utendaji wao wa kazi pamoja na kutoa elimu kwa watanzania.
Watoa huduma wakiwa tayari kutoa maelekezo kwa wananchi watakaotembelea banda lao kayika maonyesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam |
Afisa huyo amesema kuwa katika kazi zao za
kushughulika na kesi mbalimbali mkusanyiko mkubwa kesi umekuwa katika kesi za
ardhi na kesi za madai ambapo amesema kuwa kunahitajika nguvu ya ziada katika
kushughulika na kesi kama hizo kwani zimekuwa ndio nyingi kwa watanzania.
Mwanasheria kutoka LHRC ndugu HAROLD SUNGUSIA akitoa maelezo kwa wanahabari waliotembelea banda lao juu ya report hizo mbili zilizozinduliwa katika maonyesho hayo |
Akizitaja changamoto ambazo wanakumbana nazo katika
kutoa msaada wa kisheria ameseama kuwa elimu ndogo ya kisheria kwa wanachi,watu
kuwa na hofu na mahakama zetu,mahakama chache pamoja na kucheleweshwa kwa kesi
nyingi imekuwa ni kikwazo kikubwa katika secta hiyo ya sheria hapa nchini.
Maadhimisho yato yanafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam ambapo wadau mbalimbali wa maswala ya kisheria wanakutana katika maonyesho hayo.
Wananchi wanaojitokeza katika banda hilo |
No comments:
Post a Comment