Kaimu Meneja mkuu wa Tigo Tanzania, Cecile Tiano,ameelezea
nia ya kampuni yake kuongeza uwekezaji katika mikoa ya kanda ya kaskazini kwa kiasi
cha dola za kimarekani milioni 30 alipokuwa
akiongea nawaandishi wahabari mjini Arusha.
Tiano,
aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo mwezi huu, ameisifu kanda ya kaskazini inayojumuisha
mikoa ya Arusha, Manyara, Singida, Dodoma na Kilimanjaro kuwani eneo la kibiashara na utalii
bila kusahau kuwa ni njia kuu ya kuelekea mataifa jirani.
Alifafanua kwambaTigo
inajumala ya minara 334 katika ukanda wa kaskazini ikiwemo 71 iliyojengwa mwaka
2014.Mwaka jana Tigoi lijenga jumla ya minara 312 nchi nzima.
“Mwaka huu tumepanga kujenga minara mingine
748 nchima nzima ambayo 300 itakuwa katika kanda ya kaskazini ilikuhakikisha wakazi
wa vijiji vya mikoa yote mitano wanaunganishwa na huduma zetu. Kwa wastani wadola
100,000 kila mnara, hii inamaanisha uwekezaji wazaidi ya dola milioni 75 nchi nzima
ikiwemo dola milioni 30 katika mikoa hii mitano.,"
Alisema.
“Hii
inamaanisha watu wengi zaidi watapata fursa mpya za kijamii na kiuchumi,
wakiunganishwa katika uchumi wakidunia kupitia mtandao waintaneti – na kwa kufanya
hivyo tunawawezesha kujiunga na mfumo mpya wa digital,” alisisitiza Tiano.
Kanda ya Kaskazini pia imekuwa ikinufaika kwa kiasi kikubwa na mipango kadha ya udhamini na miradi ya kijami ikutoka Tigo, miradi ambayo Tiano alisema inalengo la kuleta mageuzi chanya katika Nyanja za elimu, afya, mazingira, ujasiriamali (ajira), sanaa na michezo.
“Kupitia
juhudi zetu kama zile za mashindano ya Tigo Ngorongoro Run, mbio ambazo zimekuwa
zikifanyika Karatu kila mwaka, kampuni yetu, pamoja na wadau wengine,tumeweza kukusanya
fedha ambazo hutumika kununulia vyandarua shuleni, vifaa vya hopitali mbalimbali
katika wilaya ya Karatu,”alisema.
Katika
hatua nyingine Tiano ametangaza udhaminiwa Tigo kwambio za marathoni za Kilimnajaro
mwaka huu kwa kiasi cha shilingi milioni 80. Mbio hizo zitafanyika tarehe 1
Machi 2015 ambapo Tigo inadhamini nusu marathoni ya kilomita 21, alisema
“Sababu
ya Tigo kujiingiza katika mashindano haya ni kuonesha nia yake ya kuendeleza sekta
ya michezo na Nyanja nyingine za kijamii na za kiuchumi katika nchi hii, ikiwa ni
pamoja na utunzaji wa mazingira.
Katika
kipindi cha miaka miwili iliyopita Tigo imekuwa ikiwekeza kwenye miundo mbinu yake
kwa wastani wa dola milioni mbili kwa wiki nchi nzima. Uwekezaji huu, kwa mujibu
wa Tiano, umesaidia kupanua mtandao wake
mpaka sehemu za vijijini; kuboresha mtandao wake hadi kufikia vipimo vya 3G hivyo
kuwa wezesha wateja kupata huduma ya Internet; kuelimisha wafanyakazi wake na kuleta
manufaa kwa jamii kwa kuwekea katika miradi ya kijamii.
Tiano aliendelea kusema kuwa
ndani ya miezi 12 iliyopita Tigo imekuwa kampuni ya kwanza kubni huduma mpya zikiwemo
kutuma na kupokea pesa kutoka Rwanda kupitia TigoPesa; kuanzisha huduma ya bure
ya Facebook kwa Kiswahili pamoja;na kuanzisha ushirikiano na kampuni nyingine za
simu nchini kuwawezesha wateja kutumaau kupokea pesa kutoka mitandao hiyo. Mafanikio
mengine ni kuwa wezesha wateja wake kuwekeana kutoa pesa kutoka akaunti zao za benki
kupitia simu zao za mkononi; kwapa wateja gawio la faida itokanyo na utunzaji fedha
zao katika akaunti zao za TigoPesa; na hivi karibuni uzinduzi wa huduma ya Tigo
music inayowapa wateja wake fursa ya kufurahia muziki bila kikomo kupitia Deezer
No comments:
Post a Comment