Sikiliza Audio Ya Taarifa Kuhusiana na Mkakati unaodaiwa kuandaliwa na CCM wa kumuua Dk. Slaa wavuja
MABERE Marando- Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chamacha Demokrasia na
Madendeleo
(Chadema), amefichua mawasiliano ya siri yanayofanywa na
vyombo
vya dola dhidi ya chama, na mkakati wa kumdhuru Katibu Mkuu, Dk.
Willibroad
Slaa.
Amesema
kuwa Idara ya Usalama wa Taifa na Makamu
Mwenyekiti
wa CCM
Taifa,
Philip Mangula, wamekuwa wakimtumia Khalid Kagenzi-mlinzi binafsi
wa Dk.
Slaa ili kurekodi na kuvujisha taarifa za vikao vya siri vya
Chadema.
“Kama
chama tumelalamikia sana serikali ya CCM kwa matumizi mabaya ya
vyombo
vya dola dhidi yetu. Sasa tumebaini wanatumia vijana wetu kunasa
taarifa
zetu.
“Kagenzi
kwa miaka miwili tumebaini amekuwa akitumika kupeleka taarifa
za
Chadema kwa usalama wa taifa. Amekiri hilo kwa maandishi na kutaja
namba za
watu wa usalama anaowasiliana nao,” amesema.
Marado
alimtuhumu Mangula kuwa imebainika anawasiliana na Kagenzi ikiwa
ni pamoja
na kumtumia fedha mara mbili, Julai 24 na Desemba 4 mwaka
jana,
kupitia simu yake ya Vodacom (anaitaja).
Kwa
mujibu wa Marandu, mlinzi huyo alipobanwa zaidi alieleza mkakati
uliokuwa
ukipangwa na watu hao wa kumwekea Dk. Slaa sumu kwenye chakula
au
kinywaji.
Amesema
kuwa wamebaini nyendo hizo hivi karibuni baada ya mlinzi huyo
kuonekana
akipanda katika gari ya afisa usalama wa mkoa wa Kinondoni
lenye
namba za usajili T213 ARS, akiwa nalo afisa msaidizi.
Marando
amefafanua kuwa watamfikisha Kagenzi polisi ili achunguzwe na
hatua
zaidi zichukulie, lakini akakataa kuweka hadharani namba za simu
na majina
ya maafisa usalama aliodai wako zaidi ya 22.
Amesema
kuwa pia wamenasa taarifa za maofisa hao za kumtumia Kagenzi
muda wa
maongezi zaidi ya shilinigi milioni saba kwa nyakati tofauti.
|
No comments:
Post a Comment