Tigo Tanzania imetangaza mgao mwingine
wa malipo kutoka kwenye mfuko wa fedha wa Tigo Pesa wenye thamani ya shilingi
bilioni 3.3 (US $ 1.8) kwa wateja wake. Mgao huu wa fedha ndio wa kwanza katika
robo wa mwaka huu.
Malipo haya ni ongezeko la asilimia 6
ukilinganisha na mgao uliopita wa bilioni 3.1 uliotolewa katika robo ya mwaka
iliyopita 2014. Ongezeko hili linaashiria ukuaji wa umaarufu wa huduma hii
pamoja na ongezeko la idadi ya watumiaji wa Tigo Pesa, kwa mujibu wa maelezo ya
Kaimu Meneja Mkuu, Cecile Tiano.
“Tunayofuraha kubwa sana tena kutangaza
ugawaji wa faida hii kwa watumiaji wetu wa Tigo Pesa. Malipo haya
yanadhihirisha moyo wetu wa kushiriki katika kuboresha hali za maisha wateja
wetu pamoja na nchi zima kwa ujumla,” alisema Tiano.
Alisema kwamba malipo haya ya robo
mwaka yatalipwa kwa watumiaji wote wa huduma ya Tigo Pesa ikiwemo mawakala
wakuu, mawakala wa reja reja na mteja mmoja mmoja.
“Tunaamini ya kwamba faida hii ya robo
ya kwanza ya mwaka 2015 itatoa nafuu ya kifedha kwa mamilioni ya wateja wa Tigo
kutokana na mahitaji na matumizi yao waliyonayo,” alisema.
Meneja Mkuu alielezea, kama ilivyokuwa
awali ya kwamba wastani ya kiwango amabacho mteja atajipatia itatokana na
kiwango ambacho atakuwa alikuwa anakihifadhi katika akaunti yake ya Tigo Pesa.
Tigo Pesa ilikuwa huduma ya kwanza ya
kifedha ya simu ya mkononi duniani kulipa mgao wa faida kwa wateja wake pale
mfuko wa fedha wa Tigo Pesa ulipozinduliwa kutoa migao yake ya fedha rasmi
mwezi Julai 2014. Mgao unaofuata war obo mwaka wa fedha wa mwezi Aprili mpaka
Juni 2015 utalipwa mwezi Julai mwaka huu, kutoka na maelezo ya Meneja Mkuu.
Mgao wa faida kutoka mfuko wa fedha wa
Tigo Pesa inaenda sambamba na tangazo la Benki Kuu lilitolewa mwezi Februari
2014. Mpaka sasa kampuni imekwisha lipa kiasi cha shilingi bilioni 23.9 kwa
watumiaji wa Tigo Pesa katika migao minne tofauti ya robo mwaka tangu kuzinduliwa kwa huduma hii Julai 2014.
No comments:
Post a Comment