CHAMA
CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa kuwa Kamati
Kuu ya Chama, chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, itakutana Mei 3-4, katika
kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama.
Katika kikao hicho cha siku mbili kitakachofanyika
jijini Dar es Salaam, pamoja na masuala mengine ya kitaifa kuhusu hali ya
kisiasa nchini kwa ujumla na mengine mahsusi yanayohusu uendeshaji wa chama, KK
itapokea taarifa, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu;
1. Maandalizi
ya Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
2. Taarifa
ya ziara ya mafunzo kwa timu za kampeni, viongozi wa serikali za mitaa na chama,
kukiandaa chama kushinda dola na kuongoza serikali baada ya uchaguzi mkuu wa
mwaka huu.
3. Taarifa
za utendaji wa chama kupitia kanda zote 10, Tanganyika na Zanzibar.
4. Taarifa
ya maendeleo ya mikakati ya kushiriki uchaguzi mkuu kwa kushirikiana na vyama 4
vinavyounda UKAWA.
5. Taarifa
za mwenendo wa shughuli ya uandikishaji wa wapiga kura (upya) katika daftari la
kudumu kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) na hatma ya
Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Imetolewa na;
Tumaini
Makene
Mkuu
wa Idara a Habari na Mawasiliano- CHADEMA
No comments:
Post a Comment