Meneja Mawasiliano ya Biashara wa Tigo Jacqueline
Nnunduma, (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa huduma
ya Simba News uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Rais wa Simba
Evans Aveva na kushoto ni Mkurugenzi wa EAG Group LTD, Iman Kajula ambaye ni
Mshauri wa kutekeleza shughuli za Kibiashara na Masoko katika Klabu ya Simba.
Kampuni ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na klabu ya
mpira wa miguu ya Simba wamezindua huduma ya ujumbe mfupi ijulikanayo kama
'Simba SMS', ambayo lengo lake nikuwapatia wateja wa Tigo taarifa zinazoihusu klabu
ya Simba popote walipo nchini.
Huduma
hii mpya inajulikana kama 'SIMBA SMS'. Njia hii ni rahisi na yenye ufanisi
yenye kuifanya dunia ijulikane kwa wateja wake. "Pamoja na kasi yaukuaji wa
Tehama, Tigo inaelewa umuhimu wakutoa taarifa kwa wateja wake, ndiyo maana leo,
tunajisikia fahari kuzindua huduma hii iliyotengenezwa vizuri ya SIMBA SMS
nawashirika wetu wa klabu ya SIMBA pamoja na Premier Mobile Solutions (PMS),
ilikuendelea kuwapa wateja wetu taarifa zinazohusu masuala ya sasa huku wakifurahia
habari mpya zinazohusu klabu,"alisema meneja wa mawasiliano ya kibiashara
Jacqueline Nnunduma.
Lengo letu si tukuwapatia wateja wetu taarifa kiurahisi
zaidi, lakini pia kuwapatia taarifa hizo kwa wakati na zenye uhakika kutoka vyanzo
vya michezo vyenye kuaminika," aliongeza Nnunduma.
Akizungumza
kwa niaba ya Klabu ya Simba,Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva alisema,
"Tunaamini ubunifu huu bila shaka utawawezesha mashabiki wote wa Simba na wa
soka kwa ujumla ambao pia ni wateja wa Tigo kupata habari mbalimbali za klabu ya
Simba kupitia simu zao za mkononi”.
Tunawahimiza mashabiki wetu kujiunga na huduma hii kupitia
Tigo ili waweze kupata nakufurahia habari mbalimbali kutoka klabu ya Simba.
Aliendelea Aveva.
Akiongea
katika tukio hilo Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula
ambae ni mshauri wa kutekeleza shughli za kibiashara na masoko katika klabu ya
Simba, alisema “Tunatarajia kuendelea kuwapatia mashabiki wa Simba huduma za
kisasa kwa kutumia teknolojia zisizokuwa na usumbufu wa aina yeyote kupitia wadau wanaoaminika ndani ya Tanzania”
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile
Solutions, Bi Lulu Ramole alisema kuwa huduma hii imetengenezwa ili kuwawezesha
wateja kupata habari za papo kwa papo naaliongeza kuwa huduma ipo katika mfumo wa
vifurushi vya Combo / BUNDLE PACK ambapo wateja wa Tigo watakuwa wakilipia mara
moja kwa siku na kupokea kiwango cha chini cha habari nne (04) na habari mpya za kila siku zina
zohusu klabu ya Simba.
Huduma pia itamruhusu mteja aliyejiunga kujitoa kwenye
huduma hii wakati wowote akitaka bila vikwazo vyovyote na pia kwenye huduma hii
kutakuwepo na neon kuu “MSAADA”kwa ajili ya kusaidia juu ya maswali mbalimbali ya
nayo ulizwa mara kwa mara na wateja wakati wakifurahia huduma.
Ili kujiunga na
huduma hizi unatakiwa kutuma neon kuu SIMBA kwenda 15460. Utakapo jiunga tu mteja
atapokea habari kutokana na neon analolituma kila siku na atatozwa kiasi cha
shilingi za kitanzania 150 kwa siku. Na ili kujitoa kwenye huduma mteja atahitaji
kutuma neno ONDOA SIMBA kwenda 15,460.
|
No comments:
Post a Comment