Baada ya jana aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha democrasia na maendeleo chadema Mh DK WILBROAD SLAA
kumshambulia mgombea wa UKAWA ndugu EDWARD LOWASA na UKAWA kwa ujumla leo
mwenyekiti mwenza wa umoja huo JAMES MBATIA ameibuka na kujibu mapigo ya tuhuma
hizo.
Katika mkutano
uliofanyika jijini Dar es salaam ukiongozwa na mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI na
viongozi wengine kutoka ndani ya chama hicho MH MBATIA ametumia mkutano huo
kuelezea kwa kina kile alichoita ni hoja za kutunga na za kizushi zinazopandikizwa
na chama tawala kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanauvuruga umoja wa katiba ya
wananchi UKAWA kipindi hiki ambacho wanaelekea katika uchaguzi mkuu.
Hapa ni sentensi zake katika mkutano huo
Mbatia: Napenda
kuwaomba Watanzania tusimame wote kupata Katiba mpya ambayo ndiyo ajenda ya
mgombea wetu Lowassa. #MbatiaAnaongea
Mbatia: Watanzania
naomba waelewe UKAWA tunasimamia utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi,
uwajibikaji ndani ya Tanzania.
Mbatia: Wanasiasa hasa
wale wa CCM Mwakyembe na Sita, wanaotaka midahalo waje waongee na mimi
wasimsumbue Mgombea wetu Lowassa sio saizi yao.
Mbatia: Hivi ni
ashiria kwamba CCM wameshindwa hoja, mara kuleta mambo ya udini, mara wanaibua
hili mara lile. wanataka kuchafua amani yetu kwa kuigiza masuala ya dini
Mbatia: Wagombea wetu
urais walikaa na Dokta Slaa alisema mimi ni bora kuliko wote,leo hii anasema
hajawahi kutia nia,kweli?
Mbatia: Tukisema
tuibue masuala yote na kashifa za kuuzwa kwa nyumba, kuna mtu atabaki salama?
Mbatia: Eti Lowassa
akija ndani ya Ukawa atakuja na Wenyeviti wa CCM..hakuwahi kusema..kayasemea
wapi?
Mbatia: Wewe unasema
ni muadilifu ulipewa Milioni 500 mwaka 2008 unakuja kusema leo baada ya miaka
7? Tuwe wakweli.
Mbatia: Eti suala la
rushwa zaidi ya miaka 7 usiripoti halafu uje useme leo, kusema uongo ni kazi
sana.
Mbatia: Napenda
kuwaomba watanzania wote ambao ni zaidi ya milioni 46, wasiruhusu nchi yetu
ikaharibiwa na watu 100.
Mbatia: Wakenya
walisema hata kama ana makosa, walisema huyo huyo tunamtaka, wakampigia kura na
leo ni Rais wao.
Mbatia: Watu wachache
wanaotaka eti kwa lolote lile lazima waendelee kubaki madarakani, tunasema
hapana.
Mbatia: Lazima tufute
mfumo huu uondoke tuwe na Tanzania mpya.
Mbatia: Napenda
kuwaomba wale Viongozi wa dini walionewa kwa yale ya jana, wasamehe na waachane
nayo.
Mbatia: Lowassa
hajawahi kutamka kuwa nikija ndani ya UKAWA nitakuja na wabunge 50, wenyeviti
wa CCM na Makatibu nk.
Mbatia: Kama hana
faida haya mafuriko tungepata wapi? Nyota ya Lowassa inang'aa hata wafanye nini
hawamuwezi huyu jamaa
Mbatia: Hatuna haja ya
kuanza kumjadili, hiyo ni kulipasua Taifa la Tanzania kwa maslahi binafsi
Mbatia:
Kilichotusikitisha ni yeye kuhusisha watu wengine wasiohusika kwenye jamii
yetu, viongozi wa dini wenye heshima zao, acha sisi vyama vya siasa tusuguane
wenyewe.
Mbatia: Zimebaki siku
50 na kitu, haki itendeki na nchi yetu ibaki na amani siku zote
Mbatia: Anasema kaja
kupambana na Lowassa kwakuwa anagombea urais, sasa Sumaye naye anagombea urais?
Mbatia: Nimesoma barua
ya ufisadi, ufisadi ni mfumo na Lowassa wana haki ya kujielezea zaidi wakitaka
lakini hawa wanataka kututoa kwenye reli tuanze kujibizana mmoja na wengine.
No comments:
Post a Comment