Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es
Salaam Suleiman Kova amewakumbusha watanzania hususani wananchi wanaoishi
jijini Dar es Salaam kukumbuka wajibu wao wa kudumisha amani wakati wote wa mchakato
wa uchaguzi mkuu.
mchakato huo ni pamoja
na wakati wa kampeni, siku ya kupiga kura tarehe 25.10.2015 na baada ya
kutangazwa kwa matokeo mablimbali katika
ngazi za udiwani, ubunge na urais.
Kamishna ameyasema
hayo katika uwanja wa mpira wa karume
jijini dsm alipoenda kukaguwa mazoezi ya pamoja yanayowashirikisha viongozi
wa dini mbalimbali wakiwemo Masheikh, Maaskofu, mapadre wachungaji na mabalozi
wa nchi mbalimbali.
Mabalozi na
wawakilishi wa Nchi zao walioshiriki mazoezi hayo ni pamoja na Ujerumani,
Uholanzi, Urusi, na Denmark ambao Kamishna aliwashukuru kwa ushiriki wao
ulilenga kudumisha amani ya Tanzania.
kuelekea uchaguzi mkuu kwani muda huu ni mfupi sana
ukilinganisha na muda mrefu ambapo Tanzania imekuwa na amani. Wanatakiwa
washirikiane bila kujali itikadi zao au tofauti zozote zile kwa madhumini ya kudumisha
amani iliyopo.
Jeshi la Polisi
limejiandaa kikamilifu katika kulinda amani na usalama wa Nchi na kutoa onyo
kwa wale watu wachache watakaovuruga amani na usalama kwani wakibainika
watashughulikiwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria.
Katika zoezi hilo hapo
uwanja wa karume Kamishna Kova alikabidhi mipira mitano kwa Mwenyekiti wa timu
ya Amani na mshikamano Sheikh Alhad Mussa Salum ambaye pia ni Sheilk wa Mkoa wa
Dar es Salaam akisaidiwa na Mchungaji FUPE -Makamu Mwenyekiti, na Katibu wa
timu PADRE JOHN SOLOMONI ili kuwapa hamasa katika kazi yao ya pamoja iliyo
nzuri na muhimu kwa taifa hili. Aidha Kamishna alipata fursa ya kupuliza
filimbi katikati ya uwanja ikiashiria kuanzisha mazoezi kwa madhumuni ya
kuhamasisha amani na mshikamano.
Kamishna Kova
amewambia watanzania kupitia shughuli hiyo kwamba katika kipindi hiki cha
kuelekea uchaguzi mkuu "kipaumbele
cha kwanza ni amani cha pili ni amani na
cha tatu ni amani"
SULEIMAN H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment