Katika hali ya
kushangaza leo makao makuu ya chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA
kimetokea kihoja cha karne baada ya watu wanaodhaniwa kuwa wanachama wa chama
cha mapinduzi kufanya maandamano ambayo hayakufanikiwa na badala yake
kusababisha mwandishi wa gazeti la UHURU kuingia matatani baada ya kuonekana
kuambatana na vijana hao waliokuwa wanataka kuandamana kutokumtaka Edward lowasa.
Majira ya saa nne
asubuhi vijana kadhaa ambao walikuwa wamevalia sare za chama cha CHADEMA na
mabango kadhaa walionekana wakikatiza makao makuu ya chama hicho kwa mithili ya
maandamano huku wakiwa wanachukuliwa picha na mwandishi wa gazeti la UHURU
pamoja na mpiga picha wa Television ya STAR TV ambapo baada ya kufika makao
makuu ya chama hicho walinzi pamoja na maafisa wa cham hicho walijipanga na
kuwazunguka vijana hao ambao baadhi walikuwa na boda boda hali iliyowafanya
vijana hao kutawanyika kwa kukimbia na kuvua t shirt za chama hicho ambazo
walikuwa wamevalia juu ya nguo nyingine.
Baadhi ya kadi ambazo inadaiwa kukutwa nazo mwandhishi huyo |
Katika purukushani hizo
waandishi waliokuwa wanawasindikiza waandamanaji hao akiwemo mwandishi wa
gazeti la uhuru CHRISTOPHER LISSA pamoja na mpiga picha wa STAR TV waliwekwa
chini ya ulinzi wa makamanda wa chama hicho kuwa kuhusishwa na kupanga tukio
hilo ili wapate habari kuwa kuna maandamano lengo likiwa ni kukichafua chama
hicho.
Mara baada ya kuwekwa
chini ya ulinzi akiwemo mmoja kati ya vijana ambao alionekana kuchoka (TEJA)
naye alikamatwa ambapo katika maelezo yake alikiri kupokea shilingi elfu kumi
pamoja na T-SHIRT ya CHADEMA kutoka kwa vijana hao kwa lengo la kuambatana nao
katika maandamano hayo ambayo hayakuwa halali.
Mwandishi wa gazeti la
uhuru CHRISPHER LISSA wakati akitoa maelezo kwa maafisa wa chadema alisema kuwa
yeye alipokea ujumbe mfupi wa maelezo kuwa kutakuwa na maandamano kuelekea
CHADEMA kupinga alichofanyiwa DK SLAA ambapo kwa mujibu wa mwandishi huyo
aliamua kufikisha ofisini na kupangiwa kazi hiyo ya kufanya coverage katika
maandamano hayo ya leo.
Kwa mujibu wake anasema
kuwa leo aliamua kufikia kinondoni kituo cha manyanya kutafuta hao waandamaji na ndipo alipokutana na wenzake wa STAR TV na kisha
watu ambao walikuwa wamepanga kuandamana kwalifika wakiwa na gari na kushuka na
kuanza kupeana T-SHIRT za CHADEMA huku wakiwa ni kama wageni wa eneo hilo
wakiulizia makao makuu ya chama kwa watu wengine.
Anasema kuwa baada ya
kugawiana nguo za chadema huku wakiwa hawasemi wao ni kina nani na wametumwa na
nani walianza kusogea makao makuu ya chama hicho huku wakiimba na kushiria kuwa
kua kitu wanakidai,ambapo ndipo maafisa wa chama waliamua kuwaweka kati na
kufanikiwa kuzima tukio hilo.
Akizngumza na
wanahabari afisa wa chama hicho BONIFACE JACOB amesema kuwa chama kilipata
taarifa siku tatu nyuma kuwa kuna vikao vinakaa chini ya viongozi wawili wa CCM
ambao amewataja kuwa ni PAUL MAKONDA ambaye ni mkuu wa wilaya ya kinondoni
pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la ubungo DIDAS MASABUR,vikao ambavyo
vilifanyika kurasini na ndipo chama kilijipanga kwa tukio hilo la leo.
Kwa mujibu wa afisa
huyo anasema kuwa mwandishi huyo wa UHURU anahisiwa kushiriki kupanga
maandamano hayo kutokana na kukutwa na kadi zaidi ya 20 feki za chama hicho
ambazo walijipanga kujifanya kama zimerudishwa na wanachama hao kadi ambazo
mwandishi huyo amekana kuhusika nazo.
JOHN MNYIKA AKIZUNGUMZIA KIHOJA HICHO
Akizungumzia kihoja hicho leo Naibu katibu mkuu wa CHADEMA ndugu JOHN MNYIKA amesema kuwa
wanahabari huu ni muda wa kuwa makini sana na kukwepa kutumika na wanasiasa kwa
maslahi yao binafsi kwani inaweza kuwagharimu hata maisha na baadae wanasiasa
wanakuwa wametimiza lengo lao.
Mnyika anasema kuwa
zipo mbinu chafu ambazo zinachezwa na wasiasa hasa wa chama cha mapinduzi
kuwapanga vijana na kuwataka waandamane kwa malipo na kujifanya wao ni wanachadema
jambo ambalo amesema kuwa ni kuwaumiza vijana hao kwani wamekuwa wakiishia
kupata vipigo kutoka kwa wananchi ambao wanachukizwa na vitendo hivyo.
CHINI MWANDISHI WA UHURU AKIFAFANUA
CHINI MWANDISHI WA UHURU AKIFAFANUA
No comments:
Post a Comment