1-Maeneo kadhaa ya nchi
ya Tanzania hata baada ya zoezi la
kupiga kura waliendelea kupiga kura hata
baada ya muda kumalizika lakini wengi walimaliza kwa muda husika
2-Swala la kuhesabu
kura—90% kura ziolihesabiwa vituoni lakini asilimia moja hazikuhesabiwa vituoni
3-Swala lingine ambalo
limerepotiwa na mawakala wetu walioko nchi nzima ni kuwa 99% ya mawakala wa
vyama vinavyoshiriki uchaguzi huu waliruhusiwa kuwepo kwa mujibu wa sheria
wakati wa kuhesabu kura.
4-Pia 99% wa ccm na Chadema
walikubaliana na matokeo na kutia saini katika nakala za matokeo.
5-Wakati wa zoezi la
uhesabuji kura vijana waliokuwa wanasubiri matokeo katika mitaa mbalimbali ya
nchi walikabiliana na polisi na mabomu tukio ambalo pia leo limejitokeza katika
maeneo ya Temeke ambapo baada ya wasimamizi kuchelewesha matokeo kubandika
wananchi walikusanyika na kutaka kupewa matokeo yao jambo ambali lililazimu
polisi kuwatawanya kwa mabomu.
6-Mchana wa leo pia
huko Zanzibar mabomu yamepigwa kutokana na sakata ambalo limeibuka leo ambapo
mgombea wa chama cha wananchi CUF MAALIM SEIF SHARIF HAMAD alitangaza kuwa
ameshinda uchaguzi huo kutokana na matokeo ambayo ameletewa na mawakala wa chama
chake hivyo watu kulipuka na furaha hali ambayo imezua tafrani huko Zanzibar.
7-Nia rai yetu kuwa
zoezi la uhesabuji wa kura likafanyika kwa umakini mkubwa na ili kuepusha fujo
na hiyo inasababisha watu kukosa uvumilivu na kujitangazia matokeo wenyewe na
kusababisha rapsha mitaani
8-Tunaomba hali ya
utulivu na amani lakini tukumbuke kuwa haki ndio tunda la amani na kuelewana.
9-Swala la kujumlisha
matokeo sio baya ila kujitangazia matokeo ni mbaya sana kwa sababu wanakuwa
wanachochea uvunjifu wa amani.
10-Tuhuma mbalimbali za
kukamatwa kwa mabox zinazoenea katika maeneo mbalimbali zinasemwa lakini hakuna
ushahidi wa kujitosheleza sana kumtia mtu hatiani kwa sababu tume wamekanusha
na kusema kuwa hao watu ni wafanyakazi wa kawaida wa serikali na tume hivyo ni
kutokuelewa tu mfano lile tukio la vunjo halijapata udhibitisho.
11-Tatizo ni kwamba
wafanyakazi wa tume wanapewa vifaa vya uchaguzi lakini hawapewi usafiri wa
kubebea hivyo wanalazimika kubeba na kulala navyo nyumbani hivyo ni hatari sana
kwa wafanyakazi hao.
No comments:
Post a Comment