Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempongeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
Monday, November 30, 2015
Lipumba Afika Ikulu Kumpongeza Rais Magufuli Kwa Ushindi wa kishindo
BILIONI 4 ZA SHEREHE ZA UHURU KUPANUA BARABARA YA MWENGE-MOROCO YENYE UREFU WA KILOMITA 4.3
JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA WATUHUMIWA KUMI NA MBILI WA WIZI WA MAKONTENA.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Bw.Diwani Athumani (CP) alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uchunguzi wa watuhumiwa wa wizi wa makontena kwa Mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Zitto Kabwe aibua tena Ufisadi wa $600m,soma story nzima hapa
Ufisadi wa $600m hati fungani za Serikali: Tusikubali ya Rada, hatua zichukuliwe
Taasisi ya Serious Fraud Office ya Uingereza ( SFO ) inafanya mazungumzo na Benki ya Standard Group ya Afrika ya Kusini Lakini iliyoorodheshwa katika soko la hisa ya Uingereza ( London Stock Exchange ) ili kumalizana kuhusu tuhuma za rushwa katika ununuzi wa hati fungani za Serikali ya Tanzania yenye thamani ya dola za kimarekani milioni Mia Sita ( $ 600m ). Mazungumzo hayo yanafanywa mbele ya Jaji katika mji wa London.
RAIS DKT. MAGUFULI, WAZIRI MKUU MAJALIWA, WAMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA OFISINI KWAKE IKULU DAR.

U15 YAKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA
Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya vijana, Ole Gabriel amewashukuru TFF kwa kuwekeza katika soka la vijana, na kusema mafaniko yote yanandaliwa chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua kuwalea na kuwaendeleza vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya baadae.
Sunday, November 29, 2015
Breakin newzz--SHEKH PONDA AACHIWA HURU

WAFANYAKAZI WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WAFANYA BONANZA LA KUMUAGA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU, WATWAA KOMBE
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya VPO Sports Club, Nehemia Mandia, baada ya kuibuka na ushindi katika Bonanza maalum la kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati 5-4. Picha na OMR
TUMEDHAMIRIA KUWATUMIKIA WATANZANIA – MAJALIWA
Saturday, November 28, 2015
NI HUZUNI--SAFARI YA MWISHO YA KAMANDA ALPHONCE MAWAZO
Mwili wa marehemu Alphonce Mawazo ikiwasili nyumbani kwa baba mdogo (Charles Lugiko) Nyegezi jijini Mwanza ukitokea Hospital ya Bungando kwaajili ya ibada fupi.

Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita Alphonce Mawazo ukitolewa Hospital ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba Mdogo ( Charles Lugiko) huko Nyegezi na kurudi katika viwanja vya Furahisha ili kupata heshima za mwisho kitaifa.



Familia ya Marehemu Alphonce Mawazo wakiendeshwa na mchungaji kwa ibaa fupi iliyofanyika nyumbani kwa baba Mdogo wa Marehemu.
AMOS MAKALLA APIGA MARUFUKU LIKIZO ZA MA DC, WAKURUGENZI NA WAKUU WA IDARA MKOANI KILIMANJARO
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
KATIKA hali inayoonyesha ni joto kali la kuwatumikia Watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla, amepiga marufuku likizo za Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kwenye mkoa wake ili kutekeleza kwa vitendo hotuba na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.
RC Makalla aliyasema hayo juzi katika kikao cha kazi na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa idara wa halmashauri na Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa huo kwa ajili ya kupeana mikakati ya majukumu ya kuwatumikia Wana Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla, ikiwa ni hatua nzuri ya kwenda na kasi ya Dr Magufuli.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla, akizungumza na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara katika Mkoa huo ili kujipanga katika majukumu mbalimbali ya kuwatumikia wana Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Baadhi ya watendaji wa Mkoa Kilimanjaro wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa huo, Aamos Makalla alipozungumza nao jana. Katika kikao hicho, RC Makalla alipiga marufuku likizo kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara ili kujipanga na maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.
CHANZO CHA MAJI CHA RUVU CHINI KUWATUA AKINA MAMA NDOO ZA MAJI.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Friday, November 27, 2015
Kleyah aachia video ya Msobe Msobe
MWANAMUZIKI KLEYAH AZINDUA VIDEO YAKE MPYA YA MZOBE MZOBE ALIYOMSHIRIKISHA BARNABA BOY
Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi kipya Maarufu kama bongo fleva KLEYAH ambaye anakuja kwa kasi katika Tasnia hiyo hatimaye amezindua nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la MZOBE MZOBE wimbo aliomshirikisha msanii maarufu maarufu kutoka THT Barnaba Boy CLASSIC nyimbo ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la musiki wa Tanzania.
KLEYAH ambaye ni Mhitimu wa shahada ya mawasiliano kutoka chuo kikuu cha cha Phoenix nchini marekani na baadae kufanya kazi katika shirika la kimataifa la UNDP kabla ya kuacha na kuamua kurejea nchini kwa ajili ya kuendeleza na kukuza sanaa yake Tayari amefanikiwa kufanya kazi na watayarishaji na wasanii wakubwa ambapo mwaka 2014 alifanikiwa kufanya nyimbo mbili ambazo zilirekodiwa nchini Kenya na mtayarishaji maarufu nchini humo Lucas Bikedo pamoja na kufanyia Video kwa watayarishaji maarufu nchini Kenya kwa sasa OGOPA DJS.
Katika nyimbo yake mpya ambayo ilizinduliwa Tarehe 6 Mwezi November na kuchezwa katika vituo mbalimbali vya Radio nchini Tanzania na Africa mashariki kwa ujumla na hatimaye leo umefanyika uzinduzi wa Video yake ya wimbo wa MZOBE MZOOBE unataraji kutambulishwa katika vituo mbalimbali vya Televission kwa ajili ya kumtambulisha msanii huyo ambaye anaonekana kuja kwa kasi katika sanaa hii ya music wa kizazi kipya.
Akizungumza nara Baada ya uzinduzi wa Video yake msanii KLEYAH amesema kuwa kwa sasa mipango yake ni kuendelea kufanya kazi pamoja na watayarishaji wakubwa nchini Tanzania pamoja na wasanii maarufu ili kukamilisha album yake ambayo amepanga kuizindua mwezi July mwaka 2016 album ambayo ametamba kuwa itasheheni aina mbalimbali za misic ili kuwafurahisha mashabiki wanaofwatilia kazi zake.
Ameongeza aliamua kufanya music kwa kuwa ni kitu ambacho kipo ndani ya moyo wake huku akieleza kuwa kusoma na baadae kufanya music ni jambo la kuigwa na wasanii wa Tanzania kwani itamsaidia msanii kutoboa tu si ndani ya nchi lakini Barani Africa na duniani kwa ujumla
SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU HAZINA KUACHWA TUPU
KAMANDA MPINGA AZINDUA OPERESHENI PAZA SAUTI,JIJINI DAR ES SALAAM LEO
BALOZI SEFUE KUHUSU KUSIMAMISHWA KAZI KAMISHNA MKUU TRA
JK ATINGA OFISINI KWAKE LUMUMBA
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ofisini kwake Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba
Subscribe to:
Posts (Atom)