Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa, wa ACT Wazalendo, Yeremia Maganja akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Chama cha ACT Wazalendo wakimtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda mara moja kamati ya uchunguzi kwa kamati zote zilizotuhumiwa ili ukweli ubainike na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mawasiliano wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu. |
CHAMAACT- cha Wazalendo imepokea kwa masikitiko uamuzi uliofanywa
na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai, kuwahamisha
kamati Wenyeviti, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa baadhi ya Kamati za Kudumu za
Bunge uliofanywa jana tarehe 22.3.2016.
Ikumbukwe kuwa uamuzi huu wa spika unafuatia kashfa nzito ya
viongozi na wajumbe wa kamati mbalimbali za Bunge kupokea rushwa kutoka
mashirika tofauti ya umma kama
ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari
Kufuatia taarifa hiyo ya inayoiaibisha mhimili huo wenye
jukumu la kuisimamia serikali , baadhi ya wabunge akiwemo Ndugu Zitto Ruyagwa
Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama chetu cha ACT Wazalendo walimwandikia
barua za kujiuzulu Mh. Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano ili kupisha
uchunguzi ufanyike na wataobainika kupokea rushwa kuchukuliwa hatua za
kisheria.
Chama chetu kinampongeza Mbunge wetu na Wabunge wengine
waliochukua hatua ya kujiuzulu ujumbe kwenye kamati zao ili kupisha uchunguzi. Uamuzi
huo wa ndugu Zitto unakwenda sambamba na
misingi ya Chama chetu cha ACT Wazalendo ya uadilifu na uwajibikaji.
Tangu mabunge yaliyopita, kamati za Bunge zimekuwa
zikituhumiwa mara kadhaa kujihusha na vitendo vya kupokea rushwa kutoka kwa
Mashirika ya Umma, Makampuni na watu binafsi. Rai iliyotolewa mara kwa mara
huko nyuma ya kuitishwa kwa uchunguzi ili kulinda hadhi na heshima ya Bunge
ilipuuzwa na matokeo yake, kashfa hizi
zimeliondolea heshima Bunge na Wabunge.
Kwa mujibu wa Ibara ya 63(2) ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Bunge ndiyo chombo kikuu chenye madaraka kwa niaba ya
wananchi kuisimamia na kuishauri serikali na vyombo vyake vyote katika
utekelezaji wa majukumu yake. Kinapotuhumiwa kupokea rushwa, kinawezaje
chenyewe kuisimamia serikali na kuongoza mapambano dhidi ya rushwa?
Uamuzi wa kuwahamisha Kamati viongozi na wajumbe wa Kamati
zilizotuhumiwa kupokea rushwa ni sawa na kuufunika uozo na kuendeleza utamaduni
mbovu wa siku nyingi hapa nchini wa kuwahamisha au “kuwapangia kazi nyingine” viongozi na watumishi wa umma
wanaotuhumiwa kupokea rushwa au kukosa ufanisi. Kimsingi Utamaduni huu
unafifisha mapambano dhidi ya rushwa na uwajibikaji.
Chama cha ACT Wazalendo kinamtaka Spika wa Bunge la Jamhuri
wa Tanzania kuitisha mara moja uchunguzi kwa kamati zote zilizotuhumiwa ili
ukweli ubainike na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja,kuwahamisha kamati
Wabunge kamwe hakutaondoa tatizo na kulirejeshea Bunge hadhi yake.
Tunamtaka Mh. Spika kuonyesha kwa vitendo jinsi ofisi yake
inavyochukizwa na vitendo vya rushwa nchini kwa kuitisha uchunguzi utaovishirikisha
vyombo vya dola ili ukweli ujulikane.
Ndugu Yeremia Kulwa Maganja,
Mwenyekiti, Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa,
ACT Wazalendo
23/03/2016
No comments:
Post a Comment