Tuesday, May 31, 2016
Taarifa nyingine ya mapokezi ya Zitto na wabunge wa ukawa waliosimamishwa bungeni,wanaanzia Dar
Chama cha ACT wazalendo kinatarajia kumpokea mbunge na kiongozi wa Chama hicho ndugu Zitto Kabwe siku ya JumaaMosi june 4 kwa maandamano yatakayofanyika jijini Dar na kisha mkutano wa hadhara
Pia tayari Kaimu katibu mkuu ndugu Juma Sanani ameshawaandikia makatibu wakuu wa vyama vya Chadema CUF na NCCR-Mageuzi kuwaomba wabunge wao kushiriki katika mapokezi hayo pamoja na mkutano wa hadhara kabla ya ziara hiyo kuelekea mikoani
Jana kamati ya maadili na madaraka ya Bunge iliyoowahusisha wabunge wa CCM iliwafukuza wabunge saba wa vyama vya upinzani kwa sababu ya kusimamia maslahi ya wananchi kuweza kuona mijadala ya bunge moja kwa moja badala ya kuchaguliwa vipindi na serikali ya chama cha Mapinduzi
UCHAGUZI YANGA, MWISHO WA KUCHUKUA, KUREJESHA FOMU JUNI 6
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa Klabu ya Young Africans imeridhishwa na mwenendo wa wanachama kwa namna wanavyochukua na kurejesha fomu.
Katika kikao chake cha kufanya tathmini kilichoketi jioni ya leo Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Msomi Alloyce Komba kutokana na mipango yake, imesogeza mbele mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu mpaka Jumatatu Juni 6, 2016 saa 10:00 jioni. Isipokuwa Jumamosi na Jumapili ya Juni 4 na 5, 2016.
Hadi sasa wanachama tisa (9) wamechukua na kurejesha fomu. Wanachama hao ni Aaron Nyanda na Titus Osoro wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 inayotambulika serikalini hadi sasa.
Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar ambao wanawania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji. Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 25, 2016.
Fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho www.tff.or.tz
Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji. Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni tarehe 6 Juni, 2016.
MAMBO YAMEKUWA MAMBO--UKAWA NA ACT WATANGAZA MIKUTANO MIKUBWA KUWAPOKEA MASHUJAA WAO WALIOTIMULIWA BUNGENI JANA.SOMA HII YA MUDA HUU
Sakata la wabunge kadhaa wapatao Saba wa vyama vya upinzani kusimamishwa kushiriki shighuli za bunge linaendelea kugusa hisia za watanzania ambapo sasa ni zamu ya vyama vya siasa ambavyo wabunge wao wamekumbwa na sakata hilo. Vyama vya upinzani kwa umoja wao kila kimoja muda huu wametangaza kuandaa mapokezi makubwa kwa mikoa zaidi ya mmine Tanzania kuwapokea wanaowaita mashujaa wao ambao wamesimaishwa kuingia bungeni kwa Vipindi Tofauti, Katika taarifa zilizotoka wa muda huu ambazo zote zimesainiwa na Uongozi wa chama cha ACT WAZELENDO kama wahusika wakuu katika mapokezi hayo imeeleza kuwa mapokezi hayo yafanyika kwa lengo la kuwapokea wabunge na viongozi wao waliofukuzwa bungeni kwa kosa la kudai Bunge liwe Live nchini. Nimekuwekea baadhi Ya taarifa zao hapa. |
WAAMUZI WA TAIFA STARS V MISRI WATAJWA
Waamuzi wanne kutoka Gabon, ndio watakochezesha mchezo wa kimataifa kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Mapharao wa Misri utakaofanyika Jumamosi Juni 4, 2016 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni ni wa kutafuta nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Gabon ambako mwamuzi wa kati atakuwa ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric.
Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF) kuipokea timu ya taifa ya Misri inayotarajiwa kuingia kesho Juni mosi, 2016 ambako wataweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.
Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jana Mei 30,2016 ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars. Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya 1-1
DAR BREW YAZINDUA MUONEKANO MPYA WA CHIBUKU SUPER
Meneja Masoko wa Kiwanda cha Dar Brew, Oscar Shelukindo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu uzinduzi wa chupa mpya yenye ujazo wa ml 750 za bia aina ya Chibuku. Kulia ni Meneja Mauzo na Usambazaji wa kiwanda hicho, Fredy Kazindogo.
Meneja Mauzo na Usambazaji wa kiwanda hicho, Fredy Kazindogo (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Ofisa Mauzo wa Kiwanda hicho, Agripina Kusaga (kushoto), akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Taswira meza kuu. Kutoka kulia ni Ofisa Mauzo, Neema Mvungi, Meneja Mauzo na Usambazaji, Fredy Kazindogo, Meneja Masoko, Oscar Shelukindo na Ofisa Mauzo, Agripina Kusaga.
Mkutano ukiendelea.
SERIKALI KUANZISHA BAENKI YA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo mpya ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa Viwanda PMAYA The President’s Manufacure of the Year pamoja na Mwenyekiti wa Wenyeviwanda Tanzania CTI Dkt. Samwel Nyantahe katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU / HASSAN SILAYO-MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wadau mbalimbali wa CTI na kutoka Sekta ya Viwanda nchini kabla ya kutoa Tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2015 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Leodgar Tenga mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.
NAPE AMJULIA HALI BABA WA DIWANI WA CHADEMA
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile (CHASEMA) mara baada ya kuwasili kwenye hospitali ya Nyangao kumjulia hali Baba wa Diwani huyo aliyelazwa hapo. .
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipewa maelezo juu maendeleo ya hali ya Mzee Omary Nyimbile, baba wa Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile (CHADEMA) aliyelazwa katika Hospitali ya Nyangao.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimuangalia Mzee Omary Nyimbile, baba wa Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile aliyelazwa katika hospitali ya Nyangao.
………………………………………………………………………………………
UBABE NDANI YA BUNGE WAWAIBUA LHRC-WATAKA WABUNGE KUFUTIWA ADHABU MARA MOJA NA KURUDISHWA BUNGENI
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Sheria Na haki za binadamu Nchini Tanzania Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam hukusu sakata llinaloendelea Bungeni ambalo limesababisha wabunge takribani saba kufukuzwa ndani ya bunge kwa vipindi Tofauti Tofauti hapo jana |
Wakati sakata la
wabunge saba wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania jana kusimamishwa
kuingia bungeni kwa vipindi tofauti Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini
Tanzania LHRC kimelitaka bunge la Tanzania kuwarudisha bungeni wabunge hao mara
moja kwani kufanya hivyo ni kuwarudisha nyuma wananchi katika haki zao za
kuwakilishwa.
Jana bunge la Tanzania kupitia
kwa kamati ya uongozi ya bunge hilo ilitangaza rasmi kuwafungia wabunge saba wa
bunge hilo ambao wote ni kutoka vyama vya upinzani kuingia bungeni kwa vipindi
tofauti kwa kile kilichotajwa kuwa ni kitendo chao cha kufanya vurugu ndani ya
bunge wakati wa sakata la kuwatetea wanafunzi wa UDOM waliotimuliwa chuoni
Ghafla na kuzua taharuki nchini.
GELINE FUKO ni mwanasheria wa LHRC akiwa anaeleza mambo kadhaa mbele ya wanahabari muda mfupi uliopita |
Mkurugenzi mtendaji wa
kituo cha sheria na haki za binadamu nchini HELLEN KIJO BISIMBA mbele ya
wanahabari ameeleza kuwa kitendo cha bunge kuwasimamisha wabunge ambao wamechaguliwa
na wananchi ni kitendo cha kukiuka sheria na haki za msingi za uwakilishi kwa
wananchi ambao ndio wapiga kura na ukizingatia kuwa sababu zilizotajwa hazina
uzito kulinganisha na adhabu iliyotajwa.
Ameleza kuwa Naibu
spika wa bunge hilo ambaye ni mwanamke alitegemewa sana na watanzania kuwatetea
watanzania wote hususani maskini lakini kinyume na hivyo kiti chake kimekuwa
kikiongoza bunge hilo kibabe tangu lianze kwa awamu hii ya tano jambo ambalo linaleta
wasiwasi kama bunge hilo litakuwa na uwezo wa kuisimamia na kuishauri serikali
ipasavyo.
Wanahabari kazini |
Akizungunzia chanzo cha
mgogoro wa jana amesema kuwa kitendo cha serikali kuwatimua wanafunzi wa chuo
kikuu cha Dodoma bila utaratibu maalum sio kitendo cha kuungwa mkono na kila
mtanzania anayependa haki za watanzania kwani kuwepo kwao chuoni hawakujipeleka
bali walipekwa na serikali ambayo sasa imewageuka na kuwatimua.
Ameongeza kuwa kituo
hicho kwa hatua za haraka wanaitaka serikali isitishe uamuzi wake wa kuwafukuza
wanafunzi wote wa UDOM na badala yake itafute suluhu kwa njia ya Amani na
iwaadhibu wale wote watakaobanikia kuhusika na sakata hilo.
Amesema kuwa ni kitendo
kisicho cha kiungwana kilichofanywa na Naibu spika kushindwa kujadili swala
ambalo linaendelea huku wanafunzi ambao ni Zaidi ya elfu Saba kuwa katika
maeneo hatari barabarani na wengine wakiwa hawana hela ya kujikimu jambo ambalo ni hatari kwao na
kumtaka Naibu spika huyo kuwa na utu na kujali maisha ya watoto hao.
Aidha katika upande
mwingine kituo hicho kimewapongeza wabunge wote wa bunge la Tanzania ambao jana
walionyesha kugushwa na sakata hilo la wanafunzi na kuamua kutoka nje ya bunge
kushinikiza bunge kujadili kwa dharura swala hilo bila woga kitendo ambacho
kilifanywa na wabunge wa kambi zote za bunge yani wa chama tawala na wale wa
upinzani jambo ambalo wamesema linapaswa kuendelezwa kuwatetea wanafunzi hao
ambao wanateseka katika mitaa mbalimbali ya mji wa Dodoma.
Habari hii imeandaliwa na Mwandishi EXAUD MTEI-0712098645
Monday, May 30, 2016
KUTOKA MWANANCHI-PICHA INAYOONGEA
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (kulia) akimlalamikia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu ), Jenista Mhagama (kushoto) baada ya Bunge kusitishwa leo asubuhi kutokana na kutokea kwa vurugu ambapo wabunge walikuwa wakitaka bunge hilo lijadili swala la kurudishwa nyumbani kwa wanafunzi zaidi ya 7000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma. Picha na Edwin Mjwahuzi |
Maoni kutoka kwa wanasiasa mbalImbali kuhusu kilichojiri bungeni leo
Nimekukusanyia baadhi ya maoni mbalimbali ya wadau na viongozi wa kisiasa nchini kuhusu kilichojiri bungeni na kauli zao,Hapa ninaye Katibu mkuu wa chama cha ADC,ndugu DOYO HASSAN DOYO ninaye pia mwanasiasa na mwanachama wa CUF na mchambuzi wa siasa JULIUS MTATIRO na mwanaharakari MALISA GODLISEN |
DOYO HASSAN DOYO-----Nimepokea taarifa kuwa wabunge vijana mmoja wa chadema na mmoja WA act wazalendo, yaan mh, zito kabwe, na mh Halima mdee wamefungiwa kushiriki shughuli za bunge mpaka mwezi wa tisa, Huu ni hujuma dhidi ya TAIFA letu kuhusu kudai haki, ndani ya vyombo husika, pia nimepata taarifa wabunge wengine mh, tundu lissu na Ester bulaya wamesimamishwa, kitendo hiki ndyo maono ya serikali ya awamu ya tano Namna ambavyo imejiandaa kuminya democrasia ndani ya Nchi yetu, kwa kitendo hicho tunajianda na mapambano haya ambayo ukomo wake ni pale tutakapo pata fursa za kweli za kuzungumza ukweli ndani ya Nchi yetu,
MTATIRO J----Tundu Lissu na Esther Bulaya wafungiwa kuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya bunge la bajeti na bunge lijalo la mwezi wa tisa. (Kwa hiyo hawatarudi bungeni hadi mwaka 2017).
Zitto Kabwe, Pauline Gekul, Godbless Lema na Halima Mdee wamefungiwa kushiriki vikao vilivyobaki vya bajeti na John Heche amefumgiwa kuhudhuria vikao kumi mfululizo vya bajeti kuanzia leo. (Watarudi bungeni Septemba).
Huu ni uamuzi wa kamati Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge chini Mh. George Mkuchika (Mb). Asilimia 80 ya wabunge wa Kamati hii ni wana CCM.
MY TAKE;
Huu ni ujinga wa KARNE!
Africa do need strong institution and not strong people. HAPA UDIKTETA TU, WAMESHATUMBULIWA.....TUNAISOMA NAMBA!
"Tumesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge, hatuko tayari kuwa sehemu ya kupitisha maamuzi ya hovyo na kupiga mihuri maamuzi ya kunajisi nchi yetu tutakua tayari kwa adhabu yoyote bila kuogopa".-John Heche
KAULI YA KWANZA KUTOKA ACT WAZALENZO BAADA YA ZITTO NAYE KUSIMAMISHWA KUINGIA BUNGENI
Story kubwa iliyofunga siku kwa leo ni sakata la kusimisa kwa wabunge kadhaa wa upinzani kushiriki kwa shighuli za bunge kwa vipindi tofauti,Mbunge wa kungoma Mjini ZITTO KABWE ni miongoni mwa wabunge waliopo katika List hiyo ya wabunge saba ambao inasemekana chanzo ni kuchochea Vurugu Bungeni,Baada ya Zitto Kutajwa Chama anachokiongozi cha ACT WAZALENZO wametoa kauli yao ya kwanza Ambayo Nimeinukuu kutoka kwa Ado Shaibu Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano .nimekuwekea hapa |
CHAMA Cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na kitendo cha ugandamizaji wa demokrasia kilichofanywa na wabunge wa CCM kwa kuwasimamisha ubunge wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama chetu ndg. Zitto Kabwe.
Katikati ya masikitiko hayo tunafarijika kuona wabunge hao wameondolewa kwa sababu ya misimamo yao ya kutetea maslahi ya wananchi
Tungesikitishwa zaidi kama mashujaa wetu hawa wangeondolewa bungeni kwa sababu ya ulevi au wawe sehemu ya wagonga mihuri ya masuala ya hovyo hovyo yanayosimamiwa na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM)
Kwa sababu hiyo ya kusimamia maslahi ya wananchi sisi kwetu ni mashujaa na kwa maana hiyo Chama chetu kinaandaa maandamano makubwa jijini Dar Es Salaam kuwapokea mashujaa wa wananchi
MKWASA AISHITUKIA MISRI, WANYAMA NA KAZIMOTO WATOA NENO
Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba mchezo ujao kati ya Mapharao wa Misri na Taifa Stars, utakuwa ni fainali ya kuamua taifa litakalofuzu katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON hapo mwakani kutoka kundi G.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kati ya Harambee Stars ya Kenya na Taifa Stars ya Tanzania Mei 29, 2016, uliofanyika Uwanja wa Moi Kasarani, Mkwasa maarufu kama Master anasema kwa msimamo na hali ilivyo kwa sasa, “Najua Misri wanatufuatilia. Na hata Kenya kwa siku zote tatu walikuwako. Najua Misri wanahitaji sare ili wafuzu kwa fainali hizi, lakini hawataipata Tanzania.”
Mkwasa anasema mchezo dhidi ya Misri, ana uhakika vijana wake watajitahidi ili kupata matokeo mazuri baada ya Jumapili kufanya vema dhidi ya Harambee Stars waliocheza mechi hiyo mbele ya mashabiki wao wachache ambao pia hawakuchangamka kama wale wa Tanzania ambao licha ya kuwa ugenini walichangamsha mji na uwanja.
MUSA MCHEZAJI BORA WA MEI VODACOM
Mshambuliaji Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Mei 2016.
Musa katika kinganyiro hicho aliwapiku Donald Ngoma wa Yanga na Ali Nassoro wa Mgambo Shooting. Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Musa alicheza mechi zote tatu za timu yake na kufunga jumla mabao manne; mawili katika kila mechi.
Kwa kushinda tuzo hiyo ya Mei ambayo ni ya mwisho kwa msimu huu kwa wachezaji bora wa mwezi, Musa atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Washindi wengine wa tuzo hiyo ya mwezi kwa msimu huu wa 2015/2016 ambao mechi zake za mwisho zilichezwa Mei 22 mwaka huu ni Hamisi Kiiza wa Simba (Septemba), Elias Maguli wa Stand United (Oktoba), Thaban Kamusoko wa Yanga (Desemba), Shomari Kapombe wa Azam (Januari), Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari), Shiza Kichuya wa Mtibwa Sugar (Machi) na Juma Abdul wa Yanga (Aprili).
MAJALIWA AWASILI ARUSHA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii,
Profesa Jumanne Maghembe (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix
(katikati) baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha May 30,
2016 ambako May 31, 2016 anatarajiwa kufungua mkutano wa Kimataifa wa
‘Africa World Heritage’ kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha
Arusha -AICC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WABUNGE SABA WAPIGWA KUFULI BUNGENI,YUPO ZITTO,LEMA,MDEE,BULAYA NA WENGINE,ISOME HAPA KWA UNDANI WAKE
Mwenyekiti
wa kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mhe.George Huruma
Mkuchika akiwasilisha taarifa ya Kamati hiyo kuhusu uchunguzi es vitendo
vya baadhi ya wabunge kufanya vurugu.
Uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wafanyika mkoani Mtwara
Baadhi
ya wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mpango
wa kugawa bure vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito
na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki
chandarua.
Baadhi
ya watoto wa mkoani mtwara wakishindana kucheza muziki ikiwa ni sehemu
ya burudani zilizosindikiza hafla ya uzinduzi wa mpango wa kugawa bure
vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye
umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua.
Wasanii
Joe makini na Niki wa pili kutoka kundi la weusi wakitumbuiza hadhara
iliyojitokeza katika uzinduzi wa mpango wa kugawa bure vyandarua vyenye
viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya
miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Msanii
wa nyimbo za taarab isha mashauzi akiimba moja ya kibao chake wakati
akitoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria hafla
uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa
wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa
ujulikanao kama kliniki chandarua
Sunday, May 29, 2016
PICHA ZA MATUKIO STARS NA HARAMBEE
Kikosi cha kwanza cha timu ya Soka ya Tanzania -Taifa Stars kilichoanza dhidi ya Harambee Stars ya Kenya Jumapili.
BEN POL AKONGA NYOYO ZA MAELFU WA MASHABIKI KATIKA TAMASHA LA NYAMA CHOMA JIJINI DAR ES SALAAM
BEN POL akicheza na mashabiki zake jukwaani wakati wa tamasha la nyama choma katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam |
Mashabikiwa muziki wa bongo fleva wakishangilia wakati Benpol anatumbuiza kibao chake cha MOYO MASHINE |
Subscribe to:
Posts (Atom)