Tuesday, June 7, 2016

Breaking Newzz---ZITTO KABWE anatakiwa Polisi Mara moja kuanzia sasa,Hiki ndicho kinachoendelea


Harakati za siasa ambazo zimeanzishwa tena na vyama vya upinzani baada ya wabunge wao kadhaa kutimuliwa Bungeni Zimeanza kunoga ambapo baada ya Kauli kali za mbunge ZITTO KABWE juzi mkutano wake wa mabagala zimezua mjadala mkubwa sana katika midomo ya watanzania.
Mikutano hiyo ilitakiwa kuendelea leo lakini Jeshi la Polisi limepiga marufuku mikutano hiyo

Sasa habari mpya tena ni kuwa ZITTO KABWE anahitajika Polisi haraka...Moja ya kauli ya maofisa wa chama cha ACT WAZALENDO aliyoitoa muda mfupi uliopita inaeleza yafuatayo-

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametakiwa kuripoti katika kituo cha Polisi ifika kesho saa 4 asubuhi
Juni 5 akiwa katika viwanja vya Zakhiem Mbagala Zitto alielezea namna serikali ya awamu ya tano ilivyodhamiria kuminya demokrasia na kisha akaahidi kujitoa muhanga kuhakikisha uminyaji huo WA DEMOKRASIA haufanikiwi

No comments: