MALINZI
APONGEZA UONGOZI MPYA BUNGE FC
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, amepongeza
uongozi wa timu ya Bunge FC uliochaguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini
Dodoma.
Viongozi
waliochaguliwa ni Mwenyekiti Mhe. William Ngeleja (CCM); Makamu Mwenyekiti,
Mhe. Esther Matiko; Meneja wa Klabu, John Kadutu pamoja Wajumbe ambao ni Mhe.
Neema Mgaya, Mhe. Faida Bakari, Mhe. Cosato Chumi, Mhe. Anna Lupembe na Mhe.
Grace Kihwelu.
Rais
Malinzi amewatakia kila la kheri Bunge Sports Club na kuwaahidi ushirikiano
kutoka TFF katika kuendeleza klabu yao na michezo kwa ujumla.
SAMATTA
AWAKARIBISHA MASHABIKI TAIFA
Nyota
wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amewakaribisha Watanzania kuishangilia
timu ya soka ya Tanzania - Taifa Stars ambayo kesho Juni 4, 2014 itacheza dhidi
ya Misri katika mchezo wa kuwania nafasi kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON), mwaka 2017 huko Gabon.
Samatta
aliyejiunga na kambi ya timu hiyo kwenye Hoteli ya Urban Rose, iliyoko katikati
ya jiji la Dar es Salaam, kabla ya kufanya na mazoezi na wenzake kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam aliwaambia waandishi wa habari na washindi wa
promosheni ya Bia ya Kilimanjaro wanaodhamini timu hiyo kuwa shabiki ni
mchezaji wa 12 katika kuleta hamasa ya ushindi.
“Mimi
ningependa kuwakaribisha mashabiki wote wa soka kuja uwanjani kwa ajili ya
mchezo huu,” alisema Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars anayekipiga Klabu
ya Genk ya Ubelgiji. Aliyasema hayo Jumatano jioni Juni 2, 2016 kabla ya mara
baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo.
Kwa
upande wake, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, alisema kwamba kikosi chake kimekamilia
kwa wachezaji wote kuwa katika ari ya mchezo na kwamba hakuna majeruhi
yanayoweza kumzuia hata mmoja wa wachezaji wake kuitumikia timu yake hapo
kesho.
Tayari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesikia kilio cha mashabiki wa
soka, baada ya kutangaza viingilio kwa bei ya Sh 5,000 na Sh 10,000 kwa mchezo
huo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni.
Viingilio
vilivyotangazwa ni Sh. 5,000 kwa mzunguko wenye viti vya Rangi ya Chungwa,
Kijani na Bluu wakati Viti Maalumu vya alama “B” na “C” (VIP B na C),
kiingilio
ni Sh. 10,000.
Tiketi
hizo zitauzwa kwenye vituo vya Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar
es Salaam, Ukumbi wa Burudani Mbagala Dar Live, Vituo cha mafuta cha Oilcom -
Ubungo na Buguruni (Buguruni Shell) na Ofisi za Ukumbi wa burudani Bilicanas.
Kwa
siku ya Jumamosi Juni 4, 2016 tiketi zitauzwa kwenye vituo hivyo vingine vya
Mwenge, Mnazimmoja, Makumbusho, Chang’ombe na Mgahawa wa Brake Point ulioko
mkabala makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment