IKICHEZA mchezo wa pili kwenye ligi kuu
ya soka Tanzania bara msimu huu, Mbeya City Fc imefanikiwa kuvuna
pointi zote tatu muhimu baada ya kuifunga Toto Afican ya Mwanza bao 1-0
kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba.
Haruna Shamte lifunga bao hilo mapema dakika ya 7 kwa mpira wa adhabu
iliyotplewa baada ya Joseph Mahundi kuangushwa alipokuwa kijaribu
kuwatoka waalinzi wa Toto African, hii ilikuwa ni baada ya mashambulizi
mfululizo ambayo City iliyafanya kwenye lango la timu hiyo ya Mwanza
tangu kipenga cha kuanza mpira kilipopulizwa.
Raphael Daud, Kenny Ally na Joseph Mahundi walicheza vizuri kwenye
eneo la kiungo na kuifanya City kung’ara vizuri uwanjani kipindi chote
cha kwanza licha ya jitihada za mara kadhaa kutoka kwa wachezaji wa Toto
jambo lililohitimisha dakika 45 za kwanza ubao ukisoma 1-0.
Kipindi cha pili,kocha Kinnah Phiri aliwatoa Salvatory Nkulula na
Geoffrey Mlawa aliyeumia na nafasi zao kuchukuliwa Ditram Nchimbi na
Michael Kerenge mabadiliko ambayo yaliongeza nguvu ya mashambulizi kwa
City lakini kupungua kwa umakini kwenye eneo la mwisho kulihitimisha
dakika 90 bao likisalia hilo 1-0.
Mara baada mchezo huo, Kocha Phiri amewapongeza wachezaji wake kwa
kucheza vizuri, na kuwataaka kujituza na kuwa tayari kwa mchezo
mwingine mwishoni mwa juma lijalo.
“Vijana wangu wameonyesha mchezo mzuri, kama ilivyokuwa
kwenye mchezo uliopita, kitu izuri zaidi ni kuwa leo tumepata pointi
tatu, hili ni jambo jema, kwa sababu tunapata nguvu ya kupambana kwenye
mchezo ujao”.
Kwa picha zaidi za mchezo wa Toto na City nenda hapa…
No comments:
Post a Comment