BAADA ya mapumziko ya siku ya jana yaliyotolwa na kocha Kinnah Phiri
kufuatia safari ndefu ya saa nyingi kutoka kanda ya ziwa, kikosi cha
Mbeya City fc leo kimeanza mazoezi rasmi kujiweka sawa kwa ajili ya
mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Azam Fc uliopangwa
kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa siku ya jumamosi.
Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo afisa habari wa City,
Dismas Ten amesema kuwa nyota wote 30 ikiwa ni pamoja na 25 waliokuwa
nje ya jiji la Mbeya kwa takribani wiki tatu kwa ajili ya michezo ya
mwanzo wa msimu wamejumuika kwenye mazoezi ya leo kwenye uwanja wa
Sokoine kwa ajili ya matayarisho ya mchezo huo wa mwishoni mwa juma.
“Tumeanza mazoezi leo, baada ya mapumziko ya siku ya
jana,nyota wetu wote wapo ikiwa ni pamoja na wale ambao hawakusafiri na
timu kwenda Mwanza na Shinyanga kwenye michezo mitatu ya Mwanzo wa msimu
ambayo tuliikamilisha kwa kushinda miwili na suluhu moja,limekuwa ni
jambo jema kwetu kwa sababu morari imeongezeka kikosini na kila mmoja
yuko tayari kwa mchezo wa mwishomi mwa juma” alisema.
(Picha zingine za mazoezi ya leo ziko hapa: https://www.facebook.com/MbeyaCityCouncilFc
Geoffrey Mlawa, mazoezini leo, alipokuwa akijaribu kufanya mazoezi mepesi baadae ripoti ta daktari imesema haweza kucheza mchezo wa jumamosi dhidi ya Azam Fc kwa sababu bado ni majeruhi. |
Akiendelea zaidi Ten alisema kuwa huu ni msimu ambao City
imejipanga kuvunja rekodi zote ambazo ilikuwa haijawahi kuzifikia
tangu ilipopanda daraja misimu mitatu iliyopita.
“Huu ni msimu ambao kwetu utakuwa na kumbukumbu nzuri kwa
sababu tumejipanga kufuta ‘madeni’ yote tuliyokuwa nayo, tangu
tumepanda daraja tulikuwa hatukuwahi kuongoza ligi hili sasa
limeshakwisha,tunasubiri kuvunja rekodi ya kutokuzifunga Yanga na Azam
fc jambo ambalo tuna amini tunalianza wikiendi hii” alitamba.
Wakati huo huo Ten ameweka wazi kuwa mshambuliaji Geoffrey Mlawa ni
wazi ataukosa mchezo wa jumamosi dhidi ya Azam Fc kufuatia majeraha
aliyoapata kwenye mchezo dhidi ya Toto African jijini Mwanza na tayari
jopo na madaktari wa City wameshathibitisha jambo hili mble ya benchi
la ufundi.
No comments:
Post a Comment