-------------------------
Sina tatizo na hatua za Raisi kuleta 'maendeleo' kwa wananchi na kutetea 'wanyonge'.
ILA nina tatizo na kauli zake. Kuna jinsi ambavyo kama watanzania tumezoea kusemeshana na kuongeleshana.
Sisemi kwamba tuishi kwa mazoea la hasha.
Ila ni vyema mtu yeyote uangalie unasema nini na wapi kufanikiwa nini.
Mlimani City mpango wa kuijenga ulianza kipindi cha Mh. Mkapa na kumalizika kipindi cha Mh. Kikwete kama sikosei.
Leo hii kusema kwamba mradi huo ni "magodown" ni kuwaonea waliokuwepo wakati unatekelezwa.
Mosi, maamuzi ya Serikali yeyote ni ya pamoja (collective responsibility).
Kama mtu alikuwepo kwenye mabaraza yote ya mawaziri kipindi
cha Mh. Mkapa na Mh. Kikwete kipindi ambacho magodown yamejengwa basi
hawezi kuepuka ushiriki katika kudanganywa kwetu!!
Pili, sijamsikia mtu akisema barabara ambazo zimebomoka
(mfano maeneo ya Chalinze, barabara ya Mbeya, barabara za akachube nk)
ni mitaro au mito kwa sababu zilijengwa chini ya kiwango!!
Au ule mradi wa ferry kutoka Bagamoyo - Dar ni WHITE ELEPHANT.
Au kukumbushia uuzaji wa nyumba za Serikali halafu kwenda
kujenga nyingine!! Au kuhusu wale samaki wa wachina kwamba tuliingizwa
chaka.
Tatu, uongozi ni endelevu. Zaidi pale ambapo bado ni CCM
ndio kipo madarakani. Inatuchanganya wananchi tunapoambiwa tulichezewa
na kudanganywa sana huko nyuma. Nyuma tunayoijua sisi ni ya NYERERE,
MWINYI, MKAPA na KIKWETE.
"Nyuma" ya CCM. Je ni yupi kati yao alikuwa mzembe na
asiyejua kuongoza kiasi kwamba leo hii tuko hapa na magodown yetu????
Atuombe msamaha!! Kwa njia moja au nyingine ni ukweli kwamba sisi
watanzania ni majuha. Tumechezewa wakati wa hao wote wala hatukujua. Leo
angalau ametokea mtu kutuambia ukweli. Mzee Mkapa alikuwa sahihi
kutuita malofa.
Lakini najaribu kujiamiaminisha kwamba Mh. Raisi ni mtu wa kauli za utani. Mfano,
1. Kufyatua watoto
2. Siasa mpaka 2020
3. Kuwapoteza nusu walioimba kwenye mkutano
4. Kumzamisha kisimani aliyezuia watu kuchota maji 5. Kutoa matairi kwenye magari yanayovunja sheria za barabarani.
4. Kumzamisha kisimani aliyezuia watu kuchota maji 5. Kutoa matairi kwenye magari yanayovunja sheria za barabarani.
6. Polisi kutokuwa rafiki na raia.
7. Kutokusaini pensheni mtu asipokupa mkono wa salamu nk nk.
Natamani sana niamini hivyo. Ni utani tu. Naomba sana iwe hivyo.
*#TatizoNiSisi*
*Alberto Msando*
*#TatizoNiSisi*
*Alberto Msando*
No comments:
Post a Comment