Monday, October 31, 2016
LOWASSA,SUMAYE WAWEKA KAMBI DODOMA KUTETA NA WABUNGE WA UKAWA KUNUSURU WAANDISHI WA HABARI TANZANIA
Mawaziri Wakuu wa zamani ambao ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa na Frederick Sumaye wameweka kambi mjini Dodoma ili kuteta na wabunge wa Ukawa.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema kuwa wanasiasa hao wako mjini humo kwa ajili ya kufanya vikao na wabunge wa Ukawa ili kuweka mkakati na msimamo dhidi ya hoja mbalimbali zinazotarajiwa kuibuliwa katika vikao vya Bunge vinavyoanza kesho. |
RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS UHURU KENYATTA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakiongozana kwenye Ikulu ya Nairobi Oktoba 31, 2016. Rais yuko nchini Kenya kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. (PICHA NA IKULU)
POLISI WAZUIA MKUTANO WA MAALIM SEIF ULIOKUA UFANYIKE TANGA,........WAMLINDA PROFESA LIPUMBA
Wakati polisi ikizuia mkutano mkuu maalumu wa CUF uliopangwa kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad mjini Tanga jana, mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba alifanya usafi soko la Buguruni, huku akilindwa na jeshi hilo.
Lipumba alifanya kazi hiyo akitekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi. Msemaji wa CUF, Abdul Kambaya alisema haoni kama ni jambo la ajabu kwa Lipumba kufanya usafi wakati akilindwa.
“Sioni mantiki ya swali hilo, suala la kulindwa Lipumba siyo wa kwanza,” alisema
RAIS DKT MAGUFULI AWASILI NCHINI KENYA,APOKELEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS UHURU KENYATTA
Rais Dkt John Pombe Magufuli, akilakiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta alipokaribishwa Ikulu, Nairobi nchini Kenya leo. Rais Magufuli yupo nchini Kenya kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. |
Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi la Kenya, alipowasili Ikulu jijini Nairobi leo. |
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Rais wa Kenya, Mh. Willam Ruto. |
Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta, alipowasili Ikulu ya Kenya, Jijini Nairobi leo. |
Rais Dkt John Pombe Magufuli (kulia) akiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta wakipokea salamu za kijeshi, katika viwanja vya Ikulu ya Kenya, Jijini Nairobi leo. |
HAYATOU AMTEUA MALINZI KAMATI YA MAGEUZI CAF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika, Issa Hayatou ameteua
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuwa
miongoni mwa wajumbe 11 wa Kamati maalumu ya mageuzi ya muundo wa CAF
itakayokuwa na jukumu la kufanya mabadiliko mapya ya shirikisho,
imefahamika.
LIGI YA TAIFA WANAWAKE KUANZA RASMI KESHO
Ligi ya Taifa ya Wanawake inatarajiwa kuanza kesho Jumanne Novemba 1,
2016 kwa viwanja sita kuchezwa mechi za ufunguzi ingawa hafla ya
uzinduzi wa ligi hiyo utafanyika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma katika
mchezo ambao Baobao ya hapo itakapocheza na Victoria Queens ya Kagera.
Ligi hiyo ya kwanza kufanyika nchini Tanzania, lakini pia kwa nchi za
Afrika Mashariki na Kati imetokea kuvutia wadau kadhaa wakiwamo Azam Tv
ambao wamedhamini kwa kuonyesha mubashara (live), michezo hiyo 30
itakayofanyika viwanja mbalimbali hapa nchini.
Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwamo mawaziri na wabunge ambao
kwa sasa wako kwenye vikao mjini Dodoma kwa pamoja wanatarajiwa kuwa
katika hafla hiyo ambayo pilikapilika zake zinatarajiwa kuanza saa 8.00
mchana kabla ya mchezo kuanza saa 10.00 jioni kwa saa za Afrika
Mashariki.
Holland Based Duo M.A.E MUSIC RELEASE NEW SONG FEAT BARAKA DA PRINCE
When
it comes to songs about love in Bongo, you might say the topic is
hugely saturated with each and every singer trying to showcase their
singing talent.
Now M.A.E Music a group of two ladies, Martha Yoseph and Amy Elisabeth who are based in Holland have defied geographical distances and of course their passion for bongo fleva to release a brand new audio featuring Baraka Da Prince. Now we don't know about you but this one is definitely worth the listen. Be the first to listen here.
In January M.A.E Music released Kitopokolo a video in which they featured the one and only Prince Dully Sykes who also doubles up as their Producer.
The Group which comprises of Martha Elina Joseph a Tanzanian/Dutch Singer & songwriter plus Amy Elisabeth a Dutch National, is currently on a two week holiday in Dar es salaam, Tanzania.
Now M.A.E Music a group of two ladies, Martha Yoseph and Amy Elisabeth who are based in Holland have defied geographical distances and of course their passion for bongo fleva to release a brand new audio featuring Baraka Da Prince. Now we don't know about you but this one is definitely worth the listen. Be the first to listen here.
In January M.A.E Music released Kitopokolo a video in which they featured the one and only Prince Dully Sykes who also doubles up as their Producer.
The Group which comprises of Martha Elina Joseph a Tanzanian/Dutch Singer & songwriter plus Amy Elisabeth a Dutch National, is currently on a two week holiday in Dar es salaam, Tanzania.
links za nyimbo zao on youtube
MAE Music ft. Barakah da Prince - I love you: http://youtu.be/ aLOI174FymY
MAE Music ft Dully Sykes - Kitopokolo: http://youtu.be/ HTiHmLhPPZ8
Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa wiki hii kuisha Ijumaa tarehe 31 Oktoba 2016.
Mauzo ya Soko
Idadi ya mauzo imeongezeka
kwa asilimia 39% na kufikia TZS 5.3 Bilioni kutoka TZS 3.8 Bilioni wiki
iliyopita.
Idadi ya hisa zilizouzwa
na kununuliwa imeshuka kwa asilimia 91% hadi 869,453 kutoka 9.8 Milioni wiki
iliyopita.
Kampuni tatu
zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1.
CRDB kwa asilimia 51.8%
2.
TBL kwa asilimia 44.44%
3.
DCB kwa asilimia 1.22%
Ukubwa wa Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa soko umepanda
kwa asilimia 1% na kufika Trilioni 21.8 kutoka Trilioni 21.6 wiki iliyopita.
Ukubwa wa mtaji wa
makampuni ya ndani pia umepanda kwa asilimia 0.4% hadi Trilioni 8.19 kutoka
Trilioni 8.16 wiki iliyopita.
Viashiria (Indexes)
Sekta ya viwanda
imejitokeza wiki hii kuongezeka Zaidi ya pointi 26 baada ya bei ya hisa za
TBL kuongezeka kwa asilimia 0.76%:
Bei za hisa za makampuni
mengine ya ndani ziliendelea kubaki kwenye kiwango kile kile na kupelekea
viashiria vya sekta za huduma za kibenki na za kibiashara kubakia kwenye
kiwango kile kile wiki hadi wiki.
. by Exaud Msaka Habari on Scribd
Taarifa za Kifo cha Bondia wa Tanzania Thomas Mashali
Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali amefariki dunia usiku wa kuamkia leo October 31 2016 maeneo ya Kimara DSM, Taarifa zinadai kuwa alishambuliwa na wananchi baada ya madai ya kuitiwa mwizi.
Taarifa kutoka kwa Promota wake, Siraji Kaike amesema watu aliokuwa anagombana nao walimwitia mwizi na wakawa wamemshambulia na baadaye wakawa wamemtupa na bodaboda waliokuwa wanamjua Thomas Mashali walimuokota na kumpeleka hospitali ambapo baadaye zilitolewa taarifa kuwa amefariki.
SOURCE AYYO.COM
Sunday, October 30, 2016
Tigo yapanua huduma ya 4G LTE hadi Lindi na Mtwara
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles
Wateja
wa Tigo katika mikoa ya Lindi na Mtwara hivi sasa wanaweza kufurahia
kuunganishwa na intaneti ya kasi kufuatia kampuni hiyo kupanua huduma
yake ya 4G LTE katika miji hiyo ya kusini mwa Tanzania. Teknolojia ya
4G LTE ni ya kasi takribani mara tano zaidi ya teknolojia ya 3G
iliyopo katika soko kwa hivi sasa.
Saturday, October 29, 2016
Rais Magufuli Afanya Ziara Ya Kushtukiza Wizara Ya Maliasili Na Utalii Na Kushuhudia Pembe Za Ndovu 50 Zilizokamatwa
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi baada ya kukagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016.
CHADEMA Waijibu CCM.......Wadai Lowassa ni Tishio Ndo Maana Wanamwandama, Waitaka CCM Ijiandae Kuachia Madaraka 2020
Baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia msemaji wake Christopher Ole Sendeka kusema kuwa aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa, kuwa si tishio kwa CCM.
Jumamosi ya Oktoba, 29 Chadema imejibu kuwa Lowassa pamoja na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) utaendelea kuwa tishio kwa chama hicho na kwamba CCM ijiandae kuachia madaraka mwaka 2020 kwa kuwa imejipanga kuchukua dola.
KAULI YA ACT WAZALENDO KWA OLE SENDEKA NA CCM
RC -PAUL MAKONDA AONGOZA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARY JITEGEMEE JKT MGULANI JIJINI DAR ES SALAAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT Mgulani katika mahafali ya 32 yaliyofanyika jana. Makonda alikuwa mgeni rasmi. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
RC Makonda akimkabidhi cheti Mwalimu Bora wa Shule hiyo, Grace Eliyatosha Moshi.
RC Makonda akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Bora, Samuel Ndebeto.
RC Makonda akipeana mkono na mhitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Samina Rajab baada ya kumkabidhi cheti katika mahafali ya 32 kwa ushiriki wake wa masuala ya Skauti shuleni hapo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
Huyu ndiye ni Mwanafunzi Bora wa Shule hiyo, Samuel Ndebeto.
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali. Kutoka kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kigamboni, Luteni Kanali, Laurent Mgongolwa, Mkurugenzi wa Mipango ya Huduma Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Festus Mang'wela, Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee, Luteni Kanali, Robert Kessy, Mwenyekiti wa Bodi wa shule hiyo, Brigedia Generali mstaafu, Laurence Magere, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba na Mjumbe wa Bodi wa Shule hiyo, Sebastian Enosh.
Mgeni rasm Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wafanyakazi wa shule hiyo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mhitimu wa kidato cha nne akisakata rhumba kwenye mahafali hayo.
Walimu na wanafunzi wakicheza kwaito.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT wakitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Wahitimu ndani ya ukumbi.
Mgeni rasmi Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliokuwa jukwaa kuu.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
Vijana wa Skauti wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kwaya ya shule hiyo.
Friday, October 28, 2016
BENKI KUU YA TANZANIA (BoT) YACHUKUA USIMAMIZI WA BENKI YA TWIGA BAADA YA KUFILISIKA
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jioni hii kuhusu kuchukuliwa kwa benki hiyo ambayo ilikuwa ikimilikiwa na serikali kwa asilimia 100.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mabenki, Kenedy Nyoni (kushoto), akichangia jambo kwenye mkutano huo. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu, Profesa Beno Ndulu.
Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Victoria Msina (kulia), akimkaribisha Gavana Beno Ndulu kuzungumza na wanahabari. Wa pili kutoka kulia ni Kaimu Katibu wa Benki, Mustafa Ismail.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wapiga picha wakiwa kazini.
Taswira ya ukumbi huo wakati wa mkutano.
Subscribe to:
Posts (Atom)