Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki
cha Stella Marios cha Mtwara Padre, Dkt. Charles Kitima akichangia mada katika
moja ya Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere.( PICHA
KUTOKA MAKTABA)
Na: Frank Shija,
MAELEZO
27.10.2016
Uanzishwaji wa Bodi
ya Ithibati ya Wanahabari kama ilivyoainishwa katika Muswada wa Huduma za
Habari wa mwaka 2016 hautaminya uhuru wa kutafuta na kusambaza habari.
Hayo yamebainishwa na
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Marios kilichopo Mtwara Dkt.
Charles Kitima katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii leo.
Dkt. Kitima amesema
kuwa msingi wa haki ya kutafuta taarifa na kusambaza habari unatokana ibara ya
18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo watu wasiwe na hofu ya
kuwa Bodi hiyo itawaminya watu kutoa mawazo yao.
“Bodi ya Ithibati ya
Wanahabari haiwezi kuwa kizuizi cha watu kutafuta na kusambaza habari kwani
haki hiyo ipo kikatiba kupitia ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania” Alisema Dkt. Kitima
Amesema kuwa haoni
sababu yoyote ya kupinga uanzishwaji wake kwa kuwa malengo yake ni kuhakikisha
inasimamia kanuni za maadili ya wanahabari hapa nchini na kuijengea heshima
tasnia.
Aidha aliongeza kuwa
pamoja na kuanzishwa kwa Bodi hiyo hakuna maana kwamba uanzishwaji wake
utachukua majukumu ya taasisi zingine za habari zilizopo na kuongeza kuwa
waandishi wa habari duniani kote wanafanya kazi kwa kufuata miiko ya maadili ya
uandishi wa habari.
Alisema kuwa suala
kubwa kwa mwanahabari ni kuzingatia maadili na weledi wa taaluma yake ili
kutekeleza majukumu yake pasipo kusababisha usumbufu kwa mtu au kikundi
kingine
.
Bodi ya Ithibati ya
Wanahabari ipo katika muswada wa huduma za Habari sehemu ya Tatu na kuelezewa
kwa kirefu katika kifungu cha 10 hadi 20 katika muswada huo unaopatikana katika
Tovuti ya Bunge ambayo ni www.bunge.go.tz.
|
Thursday, October 27, 2016
Dkt. Kitima; Bodi ya Ithibati ya Wanahabari haitazuia uhuru wa habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment