Watanzania wametakiwa
kuhakikisha kuwa wanaishi katika njia za kumpendeza mwenyezi mungu ikiwa ni pamoja
na kuhakikisha maswala ya kuboresha hali ya jamii yanayopewa kipaumbele,kukata
tamaa,kuamrisha mema,pamoja na kukemea maovu kama mauaji ya walemavu wa ngozi
,matendo ya kijambazi,ubakaji,ikiwa ni njia ya kumuenzi Imam Hussein aliyekuwa
mbele katika kukemea mambo hayo.
Wito huo umetoleaa leo
Jijini Dar es salaam na Kiongozi mkuu wa waislam Shia Ithnasheriya Tanzania
Sheikh Hemed Jalala wakati akiongoza mamia ya waislam katika maaandamano ya Amani
Jijini Dar es salaam ya kumkumbuka Aliyekuwa Mjukuu wa Mtume Muhammad ambaye
aliuawa Kinyama na kifo chake kubakia kuwa Historia katika maisha ya waislam
Duniani.
Sheikh Jalala amesema
kuwa Imam Hussein aliwafunza watu namna ya kupinga ukandamizaji,dhuluma,katika
jamii pamoja na kutetea haki za wanyonge hivyo ni wakati wa wananchi wa Tanzania
kuanza kufwata maneno yake na kuhakikisha kuwa wanaenzi yale mema aliyoyaacha
katika jamii.
Ameongeza kuwa
matembezi ambayo wameyafanya leo yalikuwa na lengo la kuwakumbusha watanzania
kuwa na upendo umoja na mshikamano kwa kila jambo katika jamii na pia kuwapa
ujumbe waislam na wasio waislam juuu ya mambo aliyoyafanya Mjukuu huyo wa
Mtume,matembezi ambayo yemeanzia maeneo ya ilala Boma na kuishia Msikiti wa
Shia Kigogo.
No comments:
Post a Comment