Serikali ya Tanzania ya
awamu ya Tano imesema kuwa imeanza Program maalum ya miaka 10 ya kuhakikisha
kuwa k asilimia mia ya Viwanja nchini vinapimwa na kumilikishwa kwa
watanzania wakiwemo wakulima na wafugaji na ajili ya shughuli mbalimbali za uzalishaji.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania Lilian Liundi Akizngumza katika shughuli hiyo leo Jijini Dar es salaam |
Kauli hiyo imetolewa
leo Jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna wa Ardhi nchini Mary Makondo wakati
akizngumza na wanawake wakulima na wafugaji wadogo wadogo wakati wa kongamano
liliwalowakutanisha na kiongozi huyo kumkabid
Kamishna huyo amesema
kuwa Program hiyo ya miaka kumi ya upimaji na umilikaji wa ardhi kwa wakulima
na wafugaji na watanzania imeanza katika wilaya tatu mkoani morogoro wilaya za kilombero,malinyi na ulanga ambapo
wanataraji kumaliza kwa miaka mitatu katika wilaya hizo na kuhamia katika
wilaya nyingine nchini.
Mary amesema kuwa zoezi
hilo linafanyika kwa umakini mkubwa likiwa na lengo la kuipa ardhi uthamani
wake na kuwanufaisha hasa wakulima ambao sasa wataweza kutumia ardhi hiyo
katika maswala mbalimbali kama kukopa vifaa vya kilimo kwa kuwa watakuwa na
hati halali za mashamba yao na itakuwa Rahisi kusaidiwa kinyume na sasa ambapo
wakulima wengi wanatumia mashamba ambayo hayajapimwa Rasmi.
Wanawake mbalimbali wakiandamana Katika Viwanja vya TGNP wakiwa na mabago mbalimbali yenye jumbe ya changamoto zao wakati wakimkaribisha Mgeni Rasmi leo |
Kauli hiyo ya serikali
inakuja huku Takwimu mbalimbali zikionyesha kuwa ni asilimia 20 pekee ya ardhi
iliyopimwa nchini inamilikiwa na wanawake nchini jambo ambalo limekuwa kikwazo
kikubwa sana katika uzalishaji kwa wanawake hao ambapo kamishna huyo
amewakikishia wanawake kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika litasaidia katika
kuwamilikisha wanawake wengi Zaidi ardhi na kuwasaidia katika uzalishaji wake.
Aidha katika hatua
nyingine Kmishna huyo amepokea Tamko na maazimio mbalimbali ya wanawake hao Zaidi
ya mia moja nchini waliomkabidhi kwa ajili ya kuikumbusha serikali changamoo
mbalimbali walizonazo ikiwemo maswala ya umiliki wa ardhi na sharia kandamizi
ambazo zimekuwa zikiwaminya wanawake katika umiliki wa ardhi.
Zawadi kwa Mgeni Rasmi |
No comments:
Post a Comment