Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefunga rasmi Kongamano la 30 la Kimataifa la Wanasayansi Watafiti lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) lililokuwa la siku tatu Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla amewaeleza wanasayansi hao watafiti kuwa Serikali inashirikiana nao bega kwa bega katika jukumu la maendeleo hapa nchini hivyo uwepo wao ni kielelezo tosha cha maendeleo ya Taifa na watu wake hasa katika Nyanja za kiuchumi, Afya, Mazingira na mambo mengine ya kimaendeleo.
Aidha, amebainisha kuwa changamoto za magonjwa ya virusi yanayotokana na Mbu ambapo ameahidi amewahidi wanasayansi hao na Wizara yake kushirikiana nao katika kulipitia ufumbuzi.
Dk.Kigwangalla amewahakikishia Wanasayansi hao kuwa, masuala yote ya kuimalisha huduma za Maabara katika ngazi za msingi kwani suala hilo amekuwa akilifanya kila mahala anapokwenda kwenye ziara zake juu ya upatikanaji wa huduma Maabara bora kwenye sehemu za Afya.
“Nimependa maombi yenu haya juu ya kuimalisha huduma za Maabara kwenye ngazi za msingi. Suala hili nimekua nikilifuatilia kila ziara zangu kwenye vituo vya Afya na Hospitali zote hivyo nitalibeba hili na nitaendelea nalo kwa sababu nina aamini kutoa huduma za afya bila kuwa na huduma madhubuti za Maabara ni kuchezea afya za watanzania wenzetu, Ni lazima tuwe na huduma bora za Maabra zetu na suala hili tutakaa mimi na Mh. Waziri kuona namna ya kufanyia maboresho zaidi.” Amesema Dk.Kigwangalla.
Aidha, Dk. Kigwangalla aliwatunukia vyeti maalum wanasayansi Vijana walioshiriki kwenye kongamano hilo.
Kongamano hilo la siku tatu, Oktoba 4-6, awali lilizinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan ambaye pia aliwahakikishia Wanasayansi Watafiti hao kuwa Serikali inatambua mchango wao na wataendelea na juhudi za kuwalinda kwani ni nguzo muhimu ya kufikia malengo ya millennia ya ukuaji wa kiuchumi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela amesema kufikia tamati ya kongamano hilo ni ishara tosha maandalizi yake yalikuwa mazuri na washiriki wote walioshiriki wamejifunza mengi huku wakiwa ni mfano wa kuigwa kwa elimu walioipata hapo.
Nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Amerika ambapo washiriki zaidi ya 300 wameshiriki huku mada zaidi ya 220 zikiwasilisishwa na kujadiliwa kwa pamoja na wataalam hao.
Nchi ambazo zinashiriki kongamano hilo kuwa ni Afrika Kusini, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Australia, Denmark, Ubeljiji, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, Uswis, Kanada, Sweden, Norway, Marekani, Bangladesh, Thailand na wenyeji Tanzania.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia Wanasayansi watafiti (Hawapo pichani) walioshiriki kongamano la 30 Jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga kongamano hilo la siku tatu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati) wkaiwa meza kuu. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela
Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela akielezea machache kabla ya kumwalika mgeni rasmi kufunga mkutano huo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpa shada la maua mmoja wa Staff member kwa namna walivyoweza kuandaa kongamano hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi shada la maua mmoja wa wafanyakazi wa NIMR kwa namna walivyoweza kufanikisha shughuli hiyo. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpongeza mmoja wa Wanasayansi Vijana waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpongeza mmoja wa Wanasayansi Vijana waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo
NNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi tuzo mmoja wa Wanasayansi waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hino hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpongeza mmoja wa Wanasayansi Vijana waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi tuzo mmoja wa Wanasayansi waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpongeza mmoja wa Wanasayansi Vijana waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akifunga rasmi kongamano hilo. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari mara baada ya kufunga rasmi kongamano hilo la 30.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiagagana na wenyeji wake mara baada ya kumaliza kwa kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment