*Muswada wa Huduma za Habari ( Media Services bill 2016) ni HATARI*
*Zitto Kabwe,Mb*
Serikali ya awamu ya Tano imewasilisha Bungeni Muswada wa Sheria kutunga Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari. Muswada wa Sheria hiyo sasa upo mbele ya kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kuchambuliwa na kisha kuwasilishwa Bungeni. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kanuni ya 84 Kamati ya Bunge inawajibika kuutangaza muswada na kupokea maoni ya wadau mbali mbali. Kwa hakika wadau wa muswada huu ni wananchi wote kwani haki ya kupata habari ni haki ya kikatiba.
Serikali ya awamu ya Tano imewasilisha Bungeni Muswada wa Sheria kutunga Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari. Muswada wa Sheria hiyo sasa upo mbele ya kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kuchambuliwa na kisha kuwasilishwa Bungeni. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kanuni ya 84 Kamati ya Bunge inawajibika kuutangaza muswada na kupokea maoni ya wadau mbali mbali. Kwa hakika wadau wa muswada huu ni wananchi wote kwani haki ya kupata habari ni haki ya kikatiba.
Hata
hivyo, waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari na mitambo
ya kuchapisha magazeti na majarida ni makundi yatakayoathirika moja kwa
moja na muswada huu utakapokuwa sheria. Hata hivyo, muswada unapelekwa
mbio na mwenyekiti wa Kamati katishia kuwa iwapo wadau hawatatoa maoni,
Kamati yake itaendelea na kazi zake za kutunga sheria.
Kwa muda mrefu sana Waandishi wa habari na wanazuoni mbalimbali wamekuwa wakitaka kuwepo na sheria ya kusimamia tasnia ya habari. Ninaambiwa kuwa juhudi za kutunga sheria hii ni mchakato wa zaidi ya miaka 20, tangu mwaka 1993 ambapo muswada wa kusajili waandishi wa habari uliondolewa Bungeni baada ya kuwasilishwa na Dr. William Shija wakati ule akiwa Waziri wa Wizara ya Habari na Utangazaji, ambaye sasa ni marehemu.
Vile vile kumekuwa na kilio kikubwa cha vyombo vya habari
kufungiwa kwa kutumia Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ambayo inampa
mamlaka makubwa sana waziri wa Habari. Wananchi wengi na wapenda
demokrasia walitaraji kwamba sheria mpya ingeweza kuondoa sheria
kandamizi na kuweka uhuru wa vyombo vya habari ipasavyo. Hicho sicho
kilicholetwa na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli.
Muswada uliopo mbele ya kamati ya Bunge unatoa tafsiri pana
sana ya vyombo vya habari. Sehemu ya 3 ya Muswada inatamka chombo cha
habari ni pamoja na gazeti, kituo cha radio na televisheni ikiwemo
mitandao ya kijamii ( online platforms). Muswada unatamka kuwa ni lazima
‘media house’ iwe na leseni maalumu kwa ajili kufanya kazi na waandishi
wa chombo hicho ni lazima waandikishwe kwenye chombo kiitwacho
Accreditation Board ( Bodi ya Ithibati). Iwapo sheria hii itatungwa
maana yake ni kwamba mtandao kama wa jamiiforums utapaswa kuandikishwa
na watu wote wanaotoa maoni yao kwenye mtandao huo lazima wawe na
ithibati! Haitaishia hapo, bali hata blogs nk zitapaswa kuandikishwa
kama ilivyo magazeti. Hatua hii itaminya sana uhuru wa watu kupata
habari na kupashana habari. Hata uhuru wa kujieleza utaminywa sana
kupitia mitandao ya kijamii.
Muswada unataka kuwepo na sheria ya Serikali kuamua vyombo
vya habari viandike nini na vitanagze nini. Sehemu ya 7(1)(b)(iv)
inatamka wazi kwamba Waziri anaweza kuagiza chombo chochote cha habari
cha binafsi kutangaza habari Fulani au masuala Fulani yenye umuhimu kwa
Taifa. Itakumbukwa kwamba muswada uliopita ambao ulikataliwa ulitaka
ifikapo saa mbili usiku televisheni na radio zote ziungane na TBC
kutangaza taarifa ya habari. Kifungu hiki ndio kitatumika kufanya suala
hilo kwa amri ya Waziri. Kifungu hiki pia kinampa Waziri wa Habari
mamlaka ya kuelekeza chombo cha habari kutotoa habari Fulani kwa utashi
wa Waziri. Ni dhahiri kuwa huu ni ukiukwaji mkubwa sana wa uhuru wa
habari na kuwa kikwazo kikubwa kwa kazi za waandishi. Kwa kutumia
kifungu hiki Waziri wa Habari anaweza kuagiza magazeti yote yasiandike
habari za IPTL Tegeta Escrow na Waziri atakuwa ndani ya sheria.
Muswada pia unampa Waziri wa Habari mamlaka ya kutoa Masharti ya Kazi za vyombo vya habari ( Terms and Conditions ). Hii inatia nguvu kifungu hicho hapo juu kuhusu maelekezo ya habari za kutolewa na kutotolewa na vyombo vya habari.
Muswada huu umerudisha vifungu vyote kandamizi vilivyopo
kwenye sheria ya magazeti ya mwaka 1976. Kwa mfano kifungu cha 54-56
kinampa Waziri haki ya kutamka kwamba gazeti Fulani au kitabu Fulani
kisisambazwe nchini au kuzalishwa nchini. Kwenye masuala mengine
Mkurugenzi wa Habari Maelezo na Jeshi la Polisi linaweza kuingia kwa
nguvu na kuchukua mitambo inayozalisha magazeti kwa sababu tu gazeti
hilo limechapisha habari ambayo kwa maoni ya Serikali ni habari za
kichochezi. Muswada umetafsiri uchochezi kuwa ni pamoja na kuandika au
kutangaza mambo ambayo yanaweza kutafsiriwa kuwa yanaleta chuki ya
wananchi dhidi ya Serikali. Kwa kutumia kifungu hiki, mbunge wa upinzani
akihutubia na kuonyesha ufisadi Serikalini, sheria hii inaweza kutumika
kufuta vyombo vya habari vilivyoandika au kutangaza habari hiyo.
Kwa ufupi, huu ni muswada mbaya kuliko sheria ya magazeti
ya sasa. Huu muswada unairudisha nchi nyuma katika juhudi za kujenga
Taifa lenye Haki na wajibu. Ni sheria kandamizi ambazo kama Jaji Francis
Nyalali angekuwa hai angeijumuisha katika sheria 40 kandamizi. Serikali
ya awamu ya Tano imeamua kujenga Taifa lenye giza. Rais Magufuli
ameamua kukataa kata kata kuhojiwa na kukosolewa kwa kuhakikisha kuwa
anavibana vyombo vya habari nchini. Nilipata kusema huko nyuma kwamba,
Serikali ikishamaliza kuvibana vyama vya upinzani itavibana vyombo vya
habari. Utabiri ule umetimia kupitia sheria ya huduma za habari
inayoelekea kutungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dodoma, 20/10/2016
Majibu yangu Kwa HOJA za Nape Nnauye kuhusu muswada wa Huduma za habari, 2016
ZITTO KABWE
Ndugu
yangu Nape Nnauye amejibu andiko langu nililolitoa Jana kuhusu muswada
tajwa. Kama ilivyo ada ya Siasa za kijinga jinga Nape amejibu andiko
langu Kwa kunishambulia binafsi na kuweka Hoja zake mbalimbali. Mimi
sitamjibu Nape namna yake maana wenye busara wametufunza ' when they go
low go high '. Nitajibu Hoja za Nape Na sitamjibu Nape. Hata kwenye
andiko langu sikutamka neno Nape Nnauye kwani Siasa zangu sio Siasa za
mtu bali za masuala. Sitahangaika Na mtu bali Hoja ili kujenga.
#1 Hoja ya Kushirikishwa wadau: Nape anasema
" utungaji wa mswaada kuna hatua mbili za kutoa maoni.
Hatua
ya kwanza ni pale ambapo serikali inapokuwa inatengeneza mswaada husika
kabla ya kuupeleka kwenye vikao vya kiserikali kwa hatua za kuupitisha
wadau HUSHIRIKISHWA ili kutoa maoni yao. Na kwa mswaada wa Huduma za
Vyombo vya Habari ,2016 WADAU wameshirikishwa tena na ushahidi wa
maandishi wa ushiriki wao na maoni yao UPO.
Hatua
ya pili ya utoaji maoni huwa ni baada ya mswaada kusomwa mara ya KWANZA
bungeni, Mswaada husika hukabidhiwa kwa Kamati husika ya Bunge, na
ukishakabidhiwa huwa ni waraka huru kwa umma kuusoma na kutoa maoni yao(
public document) kwa Kamati ya Bunge.
Hili
pia limefanyika mpaka hatua ya wadau kuitwa na kuja Dodoma ambapo
waliomba mbele ya Kamati wapewe muda wakamilishe kazi ya kusoma na kutoa
maoni yao. Na Mwenyekiti wa Kamati Ndg. Peter Serukamba(mb) kwa uamuzi
wa Kamati ya kudumu ya Bunge wakaamua kuwaongezea muda wadau kwa wiki
moja kukamilisha kazi hiyo, shughuli inayoendelea sasa."
Majibu ya Hoja hii
Kanuni
za Bunge ( kanuni ya 84 ) zinataka kwamba Muswada ukishasomwa Kwa mara
ya kwanza Bunge lifanye MATANGAZO Kwa umma ili kuhakikisha kuwa umma
unaelewa maudhui ya muswada na kuwezesha Wananchi kutoa maoni Yao.
Muswada huu kwanza Bunge halikutoa matangazo yeyote ( Kwa Taarifa tu Ni
kwamba Hata Kamati ya Bunge ilishindwa kutoa photocopy nakala za
uchambuzi wa muswada kutoka Kwa wanasheria wa Bunge Kwa sababu Bunge
halina Fedha. Bunge halina Fedha kutoa photocopy ya nyaraka za Wabunge
kufanyia Kazi ). Wadau wote waliokuja mbele ya Kamati ya Bunge walitamka
dhahiri kwamba wamepewa Taarifa ya kutokea mbele ya Kamati Siku 2 kabla
ya vikao Na hivyo wameomba muda zaidi wa kutoa maoni Yao. Labda Ni
kutokana Na uchanga wa shughuli za Bunge, Waziri anajenga Hoja kwamba
Ushiriki ulianzia kabla.
Mtu yeyote anayejua namna Bunge linafanya Kazi
atakwambia muswada Ni muswada pale ambapo umechapishwa kwenye gazeti la
Serikali Na kusomwa mara ya kwanza Bungeni. Wadau wote waliiambia Kamati
kwamba Kwa muswada huu Ndio walikuwa wanashirikishwa Kwa mara ya kwanza
pale mbele ya Kamati. Hivyo wadau hawakushirikishwa kwenye muswada huu
tangu umesomwa Kwa Mara ya kwanza Bungeni.
Kama Serikali ina ushahidi
wowote ule kwamba kati ya Septemba Na sasa muswada huu umehusisha mdau
yeyote waweke wazi uthibitisho huo. Nyaraka zinazoonyeshwa Na Serikali
Ni za miaka ya nyuma kabla ya muswada kuwa muswada. Ushirikishaji
unaanza rasmi pale muswada upo gazetted Na umesomwa Bungeni.
#2. Hoja ya kulazimisha vyombo vya Habari nchini kujiunga na TBC:-
"Mosi
hakuna kifungu kama hicho katika muswada huu; pili, hakuna dhamira hiyo
kwenye muswada huu; na tatu, serikali haina hata wazo hilo."
Majibu ya Hoja
Itakumbukwa
kuwa muswada wa awali ulikuwa Na kifungu hiki Na wadau wakapiga kelele
sana kukataa. Ukisoma muswada huu Kwa juu juu utaweza kuona kuwa kifungu
hiki hakipo. Mtu mwenye dhamira ovu huficha huficha mambo yake. Kwenye
muswada huu mambo mengi yaliyokataliwa Na wadau sasa yamewekwa kiujanja
Kwa kuweka Mamlaka hayo Kwa Waziri mwenye dhamana ya Habari. Serikali
inaposea hakuna kifungu hicho haisemi kuna kifungu gani. Nitawaeleza
kifungu kilichowekwa ambacho ndicho kitatumika na Waziri kufanya haya
bila kuhojiwa Na mtu yeyote yule, kupitia kanuni.
Sehemu
ya 7(1)(b)(iv) inatamka wazi kwamba Waziri anaweza kuagiza chombo
chochote cha habari cha binafsi kutangaza habari Fulani au masuala
Fulani yenye umuhimu kwa Taifa.
Serikali
itatumia kifungu hiki kutekeleza jambo lile lile ambalo wadau walikataa
kuwekwa sheria Siku za nyuma. Serikali italiweka Kwa mlango wa nyuma.
Mbaya zaidi muswada unatamka wazi kwamba Waziri mwenye dhamana ataweka
TERMS and CONDITIONS Kwa
uendeshaji wa ' media houses'. Hivyo Hata wakifuta kifungu Hicho cha 7,
bado Waziri kapewa Mamlaka makubwa sana ya kuamua Chombo cha habari
kinaendeshwaji.
Ni dhahiri kwamba Waziri ama anajua haya au kawekewa
vifungu ambavyo yeye binafsi hajui tafsiri zake lakini atashangazwa
katika utekelezaji wa sheria. Kifungu cha 60(2)(a) ( Minister to make
regulations for TERMS and CONDITIONS forOPERATIONS of
licensed media house) inampa Mamlaka hayo Waziri kiasi ambacho ataweza
kuendesha vyombo vya habari atakavyo yeye. Muswada huu unamfanya Waziri
wa Habari kuwa Mhariri Mkuu wa Taifa.
#3. Mitandao ya kijamii:
"muswada
huu unakusudia kuzibana blogs na kutaja mitandao ya kijamii kama
jamiiforums kuwa nayo itatakiwa kusajiliwa. Mtu huyu ni wa kumwonea
huruma. Bahati mbaya muswada huo hauna mamlaka wala nia hiyo. Kifungu
cha 3 cha Sheria kiko wazi kuwa usajili utahusu magazeti na majarida na
machapisho yao ya mitandaoni (magazeti mtandao ya magazeti hayo rasmi na
sio mitandao yote au mingine ya kijamii kama anavyopotosha)."
Majibu ya Hoja
Muswada
uliopo mbele ya kamati ya Bunge unatoa tafsiri pana sana ya vyombo vya
habari. Sehemu ya 3 ya Muswada inatamka chombo cha habari ni pamoja na
gazeti, kituo cha radio na televisheni ikiwemo mitandao ya kijamii ( online platforms).
Napenda
umma wa Watanzania ufahamu kwamba muswada Ni wa Kiingereza. Muswada wa
Kiswahili Ni Kwa ajili tu ya kuwezesha Wabunge wasiojua kiingereza
kuweza kuelewa vifungu vya muswada. Muswada Ni wa Kiingereza, Ndio
rasmi. Mahakamani hawatatumia muswada wa Kiswahili Bali muswada rasmi.
Tafsiri ya online platforms haikuwekwa kwenye muswada. Tafsiri ya media Ndio
imeweka Hilo la online platforms. Naomba mtu yeyote aende Google Na
kuandika online platform atapata tafsiri Ni Nini. Nitsaidia kidogo hapa
”Social
media is defined as “online interactions among people in which they
create, share, and exchange information and ideas in virtual
communities, networks and their associated platform”.
Serikali itatumia tafsiri hii ya kwenye muswada kubana mitandao ya
kijamii. Hivi Watanzania mmesahau kesi ambazo Wananchi wanapewa kupitia
sheria ya cyber crime? Hivi mnasahau kuwa Rais alisema anatamani
mitandao ya kijamii Malaika washuke waizime? Malaika watashuka Kwa
kupitia muswada huu. Muswada huu una nia ovu kabisa ya kukandamiza uhuru
wa habari.
#4.
"Ipo hoja ya Waziri kupewa mamlaka kuagiza chombo chochote kutangaza
jambo lenye umuhimu kwa umma: Katika hili pia tumsamehe kwa sababu
hahudhurii vikao vya Kamati wakati wa mijadala hii. Hili limejadiliwa
kwa kina na wahusika kuelewana. Hakuna kifungu kinachompa mamlaka hayo
Waziri.
Bali
kifungu kilichopo kinaipa fursa Serikali kuvishauri/kuvielekeza(Govt
MAY) vyombo vya habari kuungana pamoja kulinda maslahi ya Taifa
kunapokuwa na jambo la muhimu kama vile nchi kuwa VITANI au majanga
makubwa. Zitto kama kijana wa Kitanzania kama haoni umuhimu wa hili basi
hakuna namna nyingine ya kumsaidia."
Majibu
Msomaji
utaona dhahiri kuwa hakuna Hoja ya kujibu hapo. Hivi CNN inaagizwa
kisheria Na Serikali ya Marekani kuhusu kulinda Nchi Yao? Hivi hapa
Tanzania kuna Chombo cha habari binafsi ambacho kinaweza kwenda kinyume
Na Nchi wakati wa vita? Muswada umetaja vita? Maelezo ya Waziri
yanaonyesha dhahiri kuwa Serikali haina Hoja bali inahangaika kuokoteza
Hoja. Kwenye hili Sina la kujibu majibu yamo ndani ya maelezo Yao.
#4
Kwamba muswada unampa Waziri wa Habari majukumu ya kutoa masharti kwa
kazi za vyombo vya habari na kwamba anaweza kuamua gazeti lichapishwe
habari aitakayo.
Majibu
Nimeeleza huko juu kuhusu Mamlaka haya ya Waziri wa Habari. Kifungu cha 60 kipo wazi sana.
#5Zitto anasema muswada huu unampa mamlaka Waziri kuzuia chapisho au kitabu fulani kisisambazwe nchini.
Ni kweli muswada umetoa mamlaka hayo lakini Zitto ameamua kutosema ukweli wote.
Muswada
unampa Waziri mamlaka hayo si kwa kila jarida au kitabu bali yale tu
ambayo yamedhihirika kuchapisha habari huku yakivunja sheria za nchi.
Kama Zitto anafikiri nchi yetu itaruhusu majarida yanayotaka
kuhamamsisha vita na uvunjifu wa amani nchini, ajue hakuna nchi
inayoruhusu mambo hayo.
Majibu
Nadhani
wenye uelewa wanaelewa maana ya hili. Sina maelezo ya kujibu hili kwani
linajitosheleza. Nani anatafsiri maslahi ya umma? Nani atafsiri kuwa
sheria za Nchi zimevunjwa Kama sio mahakama? Kwanini kabla ya Waziri
kufungia vitabu au magazeti asipate amri ya mahakama? Yeye Waziri Ni
Nani Mpaka atoe tafsiri ya kitabu Fulani au gazeti Fulani limevunja
sheria?
#6.
Zitto anazungumzia kuwepo kwa vifungu vya uchochezi akitoa tafsiri kuwa
wabunge wa upinzani watabanwa. Kwanza katika hili lazima ijulikane kuwa
kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa ukiwemo Mkataba wa Kimataifa Juu ya
Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966, masuala yote yanayohusu
kusababisha athari kwa usalama wa taifa ni ukomo unaokubalika wa uhuru
wa habari (allowable restriction to press freedom).
Majibu
Sina
maelezo katika hili. Wenye uelewa wanaelewa namna Hoja za namna hii
hutumika. Kiufupi masuala yote ya uchochezi yaliyokuwa kwenye sheria
kandamizi ya magazeti ya mwaka 1976 yamerudishwa kwenye sheria hii mpya.
Sheria hii inakwenda mbali Na kusema " Hata ukitamka jambo ambalo
linaweza kujenga chuki ya Wananchi dhidi ya Serikali Ni uchochezi ".
Mwisho
Napenda
kutoa ushauri wa bure Kwa ndg. Nape Nnauye, kwamba kujadiliana Kwa Hoja
kuna Maslahi Kwa Nchi. Wote waliosoma andiko langu wataweza
kutofautisha vijembe, dharau, kulewa madaraka Na matusi kwenye majibu ya
Nape Na Hoja kwenye andiko langu.
Katika andiko langu sikumtaja Nape
Kwa jina Kwa sababu najua anatimiza wajibu wake Kama Waziri. Katika
majibu yake kuanzia mwanzo Mpaka mwisho Ni vijembe tu. Hii inaonyesha
uwezo wetu mdogo wa kuhimili mijadala. Hii Ndio inayofanya Watanzania
tuonekane watu ambao hatukusoma au tulikwenda shule lakini
hatukuelimika.
Haiwezekani
kwamba mtu yeyote ambaye ana Hoja tofauti Na wewe atakuwa ametumwa.
Kwamba hatuna uhuru wa mawazo binafsi Na hivyo lazima tutumwe. Hii Ni
hulka mbaya sana ambao sikutegemea Kama wanasiasa vijana wanaweza
kuiendeleza. Lakini Kama kuna mtu ambaye amezoea kutumwa Hoja Ni dhahiri
kwamba anaona mwengine yeyote mwenye Hoja nyengine katumwa Pia.
Ninaamini
muswada huu Ni mbaya Na unadidimiza uhuru wa habari. Ninaamini kuwa
muswada huu Kama ulivyo haupaswi kujadiliwa Na Bunge Kwa sababu unapaswa
kuandikwa upya. Muswada huu ukipitishwa hakuna mchapishaji ( printer )
wa magazeti atakayekubali kuchapisha magazeti Kwa sababu Kwa mujibu wa
muswada Mkurugenzi wa Maelezo anaweza kuingia kwenye mtambo wowote akiwa
Na Polisi Na kuung'oa. Haya sio kwamba hayajaanza kufanyika,
yamefanyika. Wakati wa masuala ya UKUTA kuna wachapishaji walikataa
kuchapisha gazeti lolote lililokuwa na neno UKUTA. Watu wa magazeti
wanajua hili Na wanaweza kuthibitisha Kwa namna wanayoona inafaa.
Mimi nimeandika. Nimetahadharisha. Nimetimiza wajibu wangu.
Zitto Kabwe
Safarini Maputo
21/10/2016
No comments:
Post a Comment