Afisa masoko wa kampuni ya Itel Tanzania Charles Charle akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam wakati kampuni hiyo ilipofika katika shule ya msingi Airwing Primary kwa ajili ya kuta msaada wa vifaa mbalimbali vya kimasomo kwa wanafunzi wanaosoma katika kitengo maalum shuleni hapo ambapo afisa Huyo amesema kuwa kampuni ya ITEL imejipanga kuendelea kuwasaidia watoto hao wenye uhitaji maalum na wataendelea kuwasaidia kila wakati huku akiwataka watanzania wengine kuwa na moyo wa kutoa kidogo wanachopata kwa watanzania wanaohitaji msaada wao.
Aidha amesema kuwa Msaada walioleta leo una thamani ya shilingi laki Tano ambapo umenunua vifaa mbalimbali kama Mabegi kwa wanafunzi hao,madaftari,Mathematical set,na vifaa vingine vidogo vidogo kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao katika masomo yao. |
No comments:
Post a Comment