24 Novemba 2016. Dar es Salaam. Kampuni inayoongoza katika bidhaa za afya ya mdomo
Whitedent imekabidhi magari 25 ya aina ya Suzuki Alto K10 kwa washindi kutoka
mikoa mbali mbali nchini walioshiriki promosheni ya miezi mitatu iliyokuwa
inasheherekea kuadhimisha miaka 25 ya biashara hiyo.
Mkurugenzi wa Viwanda na biashara Mh OBADIA NYAGIRO ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi HAMISI SAID zawadi ya gari baada ya kuibuka mshyindi wa Tatu katika Promosheni hiyo |
Kampeni
hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi Julai mwaka huu ilitoa nafasi kwa maelfu ya
wananchi kushiriki shindano hilo kwa kukisia idadi ya pakiti za whitedent
zilizomo ndani ya moja ya magari hayo ya aina ya Suzuki yaliyokuwa yakizunguka
nchi nzima wakati wa promosheni. Washiriki walitakiwa kujaza fomu ya ushiriki
katika kipindi hicho cha promosheni na kukisia jibu sahihi ili waweze kuingia
katika droo kubwa ya kujishindia moja ya magari hayo ya Suzuki Alto 10 kabla ya
mwisho wa Oktoba mwaka huu.
Akizungumza
katika hafla ya makabidhiano jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu Uendeshaji wa
Chemi & Cotex Raja Swaminathan alisema,
“Nina furaha
leo ya kuyakabidhi magari haya kama ishara ya kusheherekea miaka 25 ya
mafanikio pamoja na jamii yetu. Tofauti na mashindano mengine yoyote, kila
mshindi atapokea gari lenye maili sifuri
pamoja na kadi yake ya usajili, bima ya mwaka mmoja, likiwa limejazwa mafuta
tenki nzima na gharama zote za kodi kulipwa. Hii haijawahi kufanyika nchini Tanzania.”
Shindano hilo lililokuwa chini
ya uangalizi mkubwa na wa makini wa Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania lilichukua
miezi mitatu na kushirikisha mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar.
"Tulitaka kila mtu awe na nafasi ya kushiriki katika
shindano hili. Bidhaa ya Whitedent ni ya
kujivunia ya Tanzania kwa Watanzania ikiwa imetengenezwa na Watanzania. Safari
ya promosheni ilipita sio mijini tu bali pia katika vijiji ili kuhakikisha kila
mtu anapata nafasi ya kushiriki,” aliongeza Raja Swaminathan, Afisa Mkuu
Uendeshaji wa Chemi & Cotex.
Mkurugenzi wa Viwanda na biashara Mh OBADIA NYAGIRO ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi Abdul Feresh zawadi ya Funguo baada ya kushinda Gari |
Inakadiriwa kuwa zaidi ya wana Afrika
mashariki milioni 14 huanza siku yao kwa kupiga mswaki kwa kutumia Whitedent.
Nchini Tanzania kupitia ukaguzi wa Nielsen wa mwaka 2012 ulionyesha kuwa
Whitedent ina asilimia 79 ya soko nchini na hupatikana katika maduka makubwa ya
bidhaa hadi kwenye vioski vidogo.
Whitedent,
inajivunia kuwa na asili ya Tanzania na ni bidhaa inayotengenezwa kwa ubora wa
hali ya juu katika kiwanda chenye vifaa vya kisasa jijini Dar es Salaam.
Vilevile dawa hii ya meno hutengenezwa kwa viwango vya kimataifa.
Washindi wanne wa zawadi ya magari waliokabidhiwa leo Jijini Dar es salaam |
“Mafanikio makubwa ya Whitedent
yanaonyesha kuwa uwezo wa viwanda nchini kwetu ni mkubwa na tuna nafasi kubwa
ya kukua na kutengeneza bidhaa bora kwa Watanzania kwa bei nafuu na pia kuweza
kuuza ulimwenguni kote. Tunajivunia kuwa katika viongozi wa mafanikio
haya,”alimalizia Swaminathan.
Hafla
ya makabidhiano ya magari imefanyika leo rasmi katika mikoa ya Dar es Salaam,
Moshi, Mbeya na Mwanza. Miongoni mwa washindi hao kutoka Dar es Salaam ni Emmanuel
Sitta, Hamisi Saidi Shabani, Abdu Idd Fereshi, na Ramadhan Khamis Ramadhan.
Washindi kutoka Mtwara, Arusha, Dodoma, Iringa na Shinyanga wanatarajia kupata
magari yao tarehe 26 Novemba na wale kutoka Kigoma, Tabora, Morogoro, Musoma na Zanzibar tarehe 29 Novemba 2016.
No comments:
Post a Comment