Maandamano hayo
yamefanyika Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa
dhehebu hilo.
Akizungumza na wanahabari
wakati wa maandano hayo ya Amani Jijini Dar es salaam Sheikh Jalala amesema
kuwa Mtume Muhammad s.a.w. ambaye wanaadhimisha kifo chake ni kiongozi ambaye alitenda
haki kwa watu wote na kuwa na huruma kwa watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote
hivyo ni jukumu la wanadamu hususani watanzania kujifunza kuishi kwa Amani na
upendo Bila kubaguana .
Sheikh Jalala amesema
kuwa lengo kuu la matembezi hayo ambayo yameanzia Boma Jijini Dar es salaam
Hadi Kigogo ni kuwaonyesha watanzania kuwa kuna haja ya kuwa na huruma ambayo
alikuwa nayo Mtume Huyo ambayo ilimfanya kuwapenda wanadamu wote wakiwemo
waislam na wakristo na kukaa nao meza moja bila kujali Imani zao,ambapo amesema
watanzania tunatakiwa kuwa na Roho hiyo ili kudumisha Amani iliyopo.
Aidha katika hatua
nyingine Sheikh Hemed Jalala ametoa wito kwa viongozi wa dini ya kiislam
wakiwemo Masheikh,Maimam kuiga huruma ya Mtume Muhammad s.a.w. kwa kukaa na wachungaji,maaskofu,mapadre,na
viongozi wa dini mbalimbali Tofauti na zao kwa lengo la kujenga umoja na
mshikamano kama wanadamu.
No comments:
Post a Comment