Na
Exaud Mtei
Wakati
Report mbalimbali za mashirika ya kibinadamu zikionyesha ongezeko la ukatili wa
watoto nchini Tanzania hatimaye Jeshi la polisi nchini kupitia dawati maalum la
Jinsia wameanza rasmi matumizi ya mbinu za kidigitali kukabiliana na hali hiyo
inayotajwa kuongezeka siku hadi siku.
Leo
Jijini Dar es salaam Jeshi la polisi kupitia kitengo maalum cha Dawati la
Jinisia wamepokea msaada wa vifaa mbalimbali vya kisayansi vya ukusanyaji wa
Takwimu kuhusu ukatili wa Kijinsia vifaaa ambavyo vimetolewa na Jukwaa la utu
wa Mtoto –Children’s Dignity Forum –CDF vifaa ambavyo vina thamani Zaidi ya million
sabini za kitanzania.
Koshuma Mtengeti ambaye ni executive Director Kutoka CDF aizngumza na wanahabari na wadau wa maswala ya Jinsia wakati wa Makabidhiano hayo leo Jijini Dar es salaam |
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo Jijini Dar es salaam Mkuu wa kitengo cha
Dawati la Jinsia nchini Tanzania Afande DCP Maria Nzuki amesema kuwa Jeshi la
polisi limekuwa kwa kipindi kirefu wakihifadhi takwimu za ukatili wa watoto
nchini kwa njia ya makaratasi lakini sasa wameanza mpango maalum wa kutumia
vifaa vya kisasa vya kuifadhi data hizo hivyo kukabidhiwa kwa vifaa hivyo leo
ni ishara ya kufungua milango kwa wadau wengine wa maswala hayo kujitolea
kukisaidia kitengo hicho ili kufanikisha lengo lake.
Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia nchini Tanzania Afande DCP Maria Nzuki akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo |
Aidha
Afande Nzuki amelishukuru shirika la UNFPA ambao ndio wanunuzi wa vifaa hivyo
lakini pia shirika la CDF ambao ndio waliofanikisha kupatikana kwa ufadhili huo
huku akiwataka kuendeleza ushirikiano na Kitengo hicho ili kufanikisha ulinzi
wa watoto nchini.
Aidha
akizungumza na wadau hao wakati wa makabidhiano hayo Koshuma Mtengeti ambaye ni
executive Director Kutoka CDF amesema kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya Zaidi
ya million 70 vimenunuliwa kwa ufadhili wa shirika la UNFPA ambavyo baadhi yake
ni Screen kubwa ya kisasa na kitaalam,Laptop za kitaalam kwa ajili ya kuhifadhi
Data hizo,na vifaa vingine vingi.
Baadhi ya Vifaa Hivyo |
Aidha
ameongeza kuwa kwa awamu hii vifaa hivyo vitaelekezwa maeneo ambayo yana
ukatili wa watoto wa hali ya juu ambapo kwa sasa vifaa hivyo vitaanza kupelekwa
maeneo ya Tarime ambapo pia ndipo shirika hilo linapojikita Zaidi kuwasaidia
watoto kuepukana na ukatili wa namna yoyote.
Mwakilisho kutoka UNFPA ambao ndio wanunuzu wa Vifaa hivyo Bi Christine Kwayu akizngumza wakati wa hafla hiyo |
Picha Ya Pamoja Baada ya makabidhiano hayo |
No comments:
Post a Comment