Jukwaa la Katiba
Tanzania leo limemtaka Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli
kwa nafasi yake kulitangazia Taifa rasmi Tarehe rasmi ya kurejeshwa kwa mchakato
wa kupata katiba mpya ikiwa ni pamoja na kuchapishwa kwa tangazo lake katika
gazeti maalum la serikali.
Kauli hiyo imetolewa
leo Jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa JUKATA Bwana Deus Kibamba wakati akizungumza
na wanahabari kuhusu maamuzi ya mkutano mkuu
uliomalizika hivi karibuni uliokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja na
wadau mbalimbali jinsi ya kurejesha mchakato wa katiba Tanzania ambao
unaoinekana kukwama,
Kibamba amesema pamoja
na maazimio mbalimbali yaliyamuliwa na wadau wa mkutano huo umeona kuwa Rais wa
Tanzania kwa nafasi yake ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kurejesha mchakato wa
katiba nchini ili watanzania waendelee na mchakato huo baaada ya kusimamishwa
kupisha uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka Juzi nchini.
Kibamba amesema kuwa Rais
pamoja na waziri husika wanawajibu wa kufufua mchakato wa katiba kwa sasa kwani
umetumia fedha nyingi za watanzania na mchakato huo haujakamilika.
Aidha kibamba amesema
kuwa mkutano huo kwa kauli moja uliamua kuchagua wajumbe mbalimbali wanaohusika
na maswala ya katiba kufanya mchakato wa kukutana na Rais wa Tanzania
kuhakikisha kuwa wanamshawishi na kumpa maoni yao kuhusu jinsi ya kufufua
mchakato huo kwani ni ukweli kuwa watanzania sasa wanahitaji katiba mpya ambapo
pia Jukata wametangaa kusaidiana na serikali katika mchakato huo wa katiba
ikiwa ni pamoja na kuhamasisha watanzania kuwa na hari tena ya kujitafutia
katiba mpya.
No comments:
Post a Comment