Aliyekuwa
Naibu Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Tatu, na Mbunge wa
Mkuranga, Adam Kighoma Ali Malima amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo akituhumiwa kumzuia Polisi
kutekeleza majukumu yake.
Malima anatuhumiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2017 eneo la Masaki karibu
na Ubalozi wa Canada jijini Dar es Salaam jana majira ya saa sita
mchana, ambapo Polisi walikuta ameegesha gari lake sehemu isiyotakuwa na
alipotakiwa kulipeleka ‘yard’ alikataa.
Polisi hao walikuwa wameambatana na maofisa wa kampuni moja ambayo ni
wakala wa kukusanya madeni, kukamata teksi bubu pamoja na kukamata
magari ambayo yan
Licha ya Malima kuelezwa ukweli kuwa hakuwa ameegesha gari sehemu
sahihi, lakini alikataa kulipeleka alikoambiwa jambo lililoibua
mtafaruku mkubwa.
Baada ya kufikishwa mahakani yeye na dereva wake, wameachiwa kwa dhamana ya TZS milioni 5
No comments:
Post a Comment