Akizindua ripoti hivyo leo jijini dar es Salaam, Mkurugenzi wa LHRC, Dk Heleni Kijo-Bisimba amesema inaonyesha kuna ukiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi kutokana na watu wengi kuuawa kwa sababu mbalimbali.
Amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni, watu kadhaa wameuawa kwa sababu mbalimbali, ikiwamo tuhuma za ushirikina na watu kujichukulia sheria mkononi.
Amesema matukio ya wananchi kujichukulia sheria mkononi nayo yamerudi kwa kasi kwani taarifa za Polisi zinaonyesha kuwa watu 479 wameuawa na wananchi wenye hasira. |
"Taarifa ya kipindi hiki inaonyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za raia hususani haki ya kuishi, lakini pia ukiukwaji mkubwa wa haki za makundi maalum hasa wanawake na watoto," amesema.
Amesema pia kuna vifo tisa ambavyo vinahusisha vyombo vya dola, ingawa Jeshi la Polisi katika taarifa yake inaonyesha ni mtu mmoja pekee ndiye aliuawa akiwa mikononi mwao.
No comments:
Post a Comment