Friday, August 25, 2017

KAMANDA MKONDYA AENDELEA KUWASHIKISHA ADABU MAJAMBAZI SOMA HAPA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata Bunduki mbili moja ikiwa ni aina ya Shotgun na ya pili ikiwa ni aina ya Browning kwa waalifu inaosadikika kuwa ni majambazi.
hayo yamesemwa mapema leo na Kaimu Kamanda Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Bw. Lukas Nkondya alipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam.

Kamanda Nkondya alisema bunduki hiyo aina ya Shotgun iliyokatwa kitako ilikamatwa kutoka kwa jambazi anayeitwa Khalid Salum Likwaulo mnamo tarehe 9/8/2017 majira ya saa 4 kamili kwenye makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere na askari waliokuwa dolia katika eneo hilo.

Aidha kamanda huyo alisema kuwa jambazi huyo aliyekuwa na pikipiki nyeusi aina ya Boxer yenye namba za usajili MC.161 AXF jambazi huyo alipoona uwepo wa askari eneo hilo aliacha pikipiki na kukimbia kwa miguu lakini polisi walifanikiwa kumkamata na baada ya kupekuliwa kwenye begi laki ndipo alipokutwa na silaha hiyo.

Lakini pia Bastora ya pili aina ya Browning ilikamatwa eneo la Tabata Chang'ombe majira ya saa 2 na nusu usiku ambapo askari walipata taarifa kuwa kuna kikundi maeneo hayo kinajiandaa kwenda kufanya uhalifu, ndipo askari wakaenda kuvamia eneo hilo na hao waalifu walipoona askari wakakimbia pasipojulikana.

Na baada ya waalifu kukimbia askari wakakagua mahali hapo na kukuta bastora hiyo aina ya Browning ikiwa na risasi nne kwenye Magazine huku namba zake zikiwa zimefutwa.

Lakini pia Kamanda Nkondya alisisitiza kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaina majambazi hao walikuwa wanaenda kuvamia wapi na ni kwanini, hivyo uchunguzi utakapokamilika watajulishwa wananchi wote..

Na kwa sasa kamanda huyo amepewa uhamisho wa kikazi kwa sasa anaenda kuwatumikia wananchi wa Mtwara kuwa ameteuliwa kuwa kamanda wa polisi wa mkoa huo, na sasa sio naibu tena bali ni kamanda wa mkoa wa Mtwara..

No comments: