Wednesday, October 25, 2017

BEN POUL AFUNGUKA KUHUSU KUSHINDWA KWAKE KUMILIKI LEBEL YA MUZIKI

Wakati wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz, Vanessa Mdee na wengine wakifungua rekodi label zao kwa ajili ya kuwasimamia wasanii, Mwanamuziki 'Ben Pol' kwa upande wake amedai kuwa hana uwezo huo kwasasa.
Image result for ben pol
Mkali huyo wa RnB anayefanya vizuri na ngoma yake 'kidume' amesema hana uwezo wa kumlipia msanii gharama za video na kudai kwamba atabaki kutoa misaada ya kawaida kwa wasanii wachanga kama kutoa connection na mambo mengine

"Mimi niwe mkweli kwasasa hivi level ya kum-manage mtu kiasi cha kulipa video na mambo mengine bado sijaweza, mimi ninachokiweza nina uwezo wa kumuandikia mtu nyimbo, kumlipia studio, kumsaidia ku-release, ku-promote, kumsaidia connection za kufanya kazi na watu wengine, kumsaidia kupata management bora ambayo ipo proper. Hivyo ndio vitu ninavyoviweza kwa sasa hivi" amesema Ben Pol

No comments: