Dhehebu la
Shia Ithnasheria nchini leo limefanya matembezi ya amani yaliyoanzia kituo cha
mabasi Ilala Boma na kuelekea mpaka msikiti Al Ghadiir uliopo Kigogo jijini Dar
es salaam, lengo likiwa ni kuenzi na kukumbuka mchango wa Imam Hussein.
Akiyazungumzia
matembezi hayo kiongozi mkuu wa Shia Ithnasheria Sheikh Hemed Jalala amesema
kuwa ni matembezi yenye faida kwa waislamu na wasiokuwa waislamu kwa kumuenzi
mjukuu wa pili wa Mtukufu Mtume Mohamad ambaye alifariki kwa kuwatetea wanadamu
bila kuangalia itikadi zao za kidini, kikabila rangi, madhehebu nk.
Aliendelea kwa
kusema kuwa ni kitendo cha ajabu sana kwa mtu kujitolea maisha yake kwa ajiri
ya watu wengine, na kwa Imam Hussein alikufa akiwa yeye na familia yake na
wengine ni watoto wadogo walio chini ya umri wa miezi sita wote waliuwawa na
hii ni katika kukomboa dunia ya leo ambayo imebujikwa na mambo mengi yasiyo
mazuri kama ugaidi, wizi, magomvi yasiyo na tija kwao.
Aidha Sheikh
Jalala alisisitiza kuwa kitendo kilichofanywa na Imam Hussein
kinatufundisha
wanadamu wa leo kujenge tabia ya kupendana, kuhurumiana, kusaidiana pamoja na
kuheshimiana bila kuangalia itikadi zetu za kidini, kisiasa, kikabila nk. Kwani
Imam Hussein alifanya ukombozi huo ili tusibaguane ila tuwe na umoja kati yetu
sisi na majirani zetu hata na marafiki zetu na watu wote tunaoishi katika jamii
moja.
Hivyo kupitia
matembezi haya watanzania watajifunza mengi kwani hii sio kwa waislam tu bali
watu wadini zote walipewa nafasi ya kujifunza mengi toka kwa Imam huyo ambaye
aliishi katika kipindi kibaya ambapo hakukuwa na upendo, amani ilitoweka lakini
yeye alisimama na kupingana na hali hiyo na siyo kwa faida yake tu bali ni kwa
dunia nzima iweze kuwa huru na watu waishi vizuri kama mapenzi ya mungu
yanavyotuamauru tufanye.
Na mwisho
alipenda kuwasisitiza Watanzania kuendelea kulinda Amani tuliyo nayo, Umoja
wetu pamoja na mshikamano na tusikubali kuvipoteza hivi vitu kwani ni nuru yetu
tuliyopewa na mungu, kwani watanzania ni watu tusiojua kubaguana kikabila,
kidini, kimaumbile hata kwa vipato vyetu bali tunaunganishwa na nguzo zetu kuu
ambazo ni Amani, Umoja na mshikamano wetu.
No comments:
Post a Comment