Saturday, December 30, 2017

NIDA YATAJA MIKOA INAYOFANYA VIZURI ZOEZI LA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Ndg Andrew W. Massawe ameitaja mikoa ya Mara, Arusha,  Iringa,  Geita,  Lindi,  Simiyu, Mbeya na Songwe kuwa mikoa inayoongoza katika zoezi la kuwasajili wananchi kupata Vitambulisho vya Taifa; huku mikoa mingine ikiwa nyuma kiusajili kulinganisha na malengo waliyowekewa.
Mhe.Dkt Mwigulu L.Nchemba akikagua baadhi  ya Vitambulisho 3470 ambavyo watagawiwa wananchi wa Kata ya Songea ambao Usajili wao umekamilika kufuatia zoezi la Usajili Vitambulisho kuwa kufanyika katika Kata za karibu kabla ya kuanza Usajili wa Umma. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme na Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida Ndugu Andrew W. Massawe.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa zoezi la usajili kwa mkoa wa Ruvuma lilofanyika katika viwanja vya Lisaboni-Songea, Ndugu Massawe amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba kusaidia kuweka msukumo kwa viongozi na wananchi kwenye mikoa ambayo haifanyi vizuri ili iongeze kasi ya usajili kwa lengo la kukamilisha usajili kwenye mikoa  yao kwa muda uliopangwa.

Akihutubia wananchi wa Ruvuma waliofurika kwenye viwanja vya Lisaboni vilivyopo nje kidogo ya mji wa Songea, Waziri wa Mambo wa Ndani ya Nchi Mhe.Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amewasisitizia wananchi kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kwani kuwa na kitambulisho cha Taifa siyo suala la hiyari ni wajibu kwa kila Mtanzania mwenye sifa kuwa nacho.

“ Mhe. Rais wetu ametoa hela za kuwasajili, zoezi ni bure bado kujisajiliwa kwenda kupigwa picha na kuchuliwa alama za vidole ikushinde?” aliuliza Waziri huyo mwenye dhamana kubwa katika kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo.
Mhe Waziri akimkabidhi Kitambulisho chake mmoja wa wananchi wa Kata ya Songea Bwana Hassan Ally Shomari wakati wa zoezi la ugawaji Vitambulisho kwenye sherehe za uzinduzi wa zoezi la Usajili kwa mkoa wa Ruvuma. Jumla ya Vitambulisho 3470 viligawanywa kwa wanachi wakati wa sherehe hizo.
Aidha amewataka viongozi wa Mikoa na wote wenye dhamana katika kusimamia zoezi hili kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika kuhakikisha wananchi wenye sifa wanasajiliwa na kamwe pasiwepo wageni watakaojipenyeza kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa kama raia.

“Kwakuwa NIDA inatoa vitambulisho vya aina tatu, cha Raia, Mgeni na Mkimbizi basi niwaombe wageni badala ya kufanya udanganyifu wajisajili kwa hadhi yao kwani siyo dhamira ya Serikali kumfukuza yeyote lakini kuwatambua Raia wake kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani” alisema

Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme amemhakikishia Mhe. Waziri mkoa wake uko tayari kusimamia na kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa na kupata Vitambulisho ndani ya muda uliopangwa na kwamba kamwe hata mvumilia mtu yeyote ambaye atakuwa kikwazo katika utekelezaji wa zoezi hilo kwa wananchi; akiwakemea wanasiasa kuingiza siasa kwenye zoezi la Usajili wananchi vitambulisho vya Taifa.

Mkoa wa Ruvuma wenye Wilaya 5 unakisiwa utawasajili zaidi ya wananchi 900,000 katika zoezi lililopangwa kumalizika ndani ya miezi mitatu. Tayari NIDA imekamilisha usambazaji wa vifaa na kutoa mafunzo kwa maafisa ambao watatumika kuwasajili wananchi wa Ruvuma na viunga vyake.
kikundi cha burudani za asili maarufu kama wana Lizombe wakitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa zoezi la Usajili kwa mkoa wa Ruvuma.

Mikoa mingine inayoendelea na Usajili kwa sasa ni Iringa,  Mbeya, Njombe,  Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Songwe, Lindi na Mtwara.

SAUTI JAMII KIPUNGUNI WAFANYA HILI KATIKA KAMPENI YAO YA KUPINGA UKEKETA KATIKA KATA HIYO

Wanaharakati wa Sauti Jamii Kipunguni wakiwa na watoto mbalimbali wa kata ya hiyo wakiwa wameshika mabango yenye jumbe tofauti tofauti kuashiria kuchoshwa na vitendo vya ukeketaji vilivyoshamili katika kata hiyo, mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya Akeketwi mtu mwaka 2018.

Watoto kutoka mitaa mbalimbali ya kata ya Kipunguni wakilifuata gari la matangazo la Sauti Jamii Kipunguni na kuzipokea kwa furaha huduma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ikiwa ni kugawa vipeperushi na kutoa elimu bure, mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya Akeketwi mtu mwaka 2018.
Mchungaji wa kanisa la Sinai Pentecostal Ndugu. Imani Juma Feruzi akibandika karatasi yenye ujumbe(posters) katika pikipiki mapema jana, katika uzinduzi wa kampeni ya akeketwi mtu mwaka 2018 iliyoandaliwa na Sauti Jamii Kipunguni ili kupinga vitendo vya Ukeketaji na Rushwa ya ngono.

Mwanaharakati wa Sauti Jamii Kipunguni Bi. Tausi Msangi akibandika karatasi yenye ujumbe(posters) katika moja ya duka la dawa linalopatikana katika kata ya kipunguni, mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya Akeketwi mtu mwaka 2018.

Mkurugenzi wa Sauti Jamii Kipunguni Bw. Selemani Bishagazi akigawa vipeperushi kwa wakazi mbalimbali wa kata ya Kipunguni eneo la Machimbo, katika uzinduzi wa kampeni ya akeketwi mtu mwaka 2018 mapema jana jijini Dar es salaam.
Wanaharakati wa kata ya kipunguni wakicheza kwa pamoja na watoto wa kata hiyo mara baada ya kuwapa elimu juu ya kupinga ukeketaji na rushwa ya ngono mapema jana jijini Dar es salaam.

Wanaharakati wa kata ya Kipunguni wakiwa katika picha ya pamoja mapema jana jijini Dar es salaam.

Na Vicent Macha

Kituo cha Sauti jamii Kipunguni jana tarehe 29 mwezi desemba kimezindua kampeni mahususi ya kutoa elimu mtaa kwa mtaa, iliyofuatiwa na zoezi la kugawa vipeperushi pamoja na kubandika karatasi zenye jumbe mbalimbali katika kata hiyo.

Akiongoza kampeni hiyo Mkurugenzi wa Sauti jamii Kipunguni Bw. Selemani Bishagazi alisema kuwa lengo kuu la kampeni hiyo kuangazia sehemu kuu mbili ambazo ni kupinga ukeketaji katika kata hiyo lakini pia rushwa ya ngono katika jamii ya kitanzania.

Aidha Bw. Bishagazi alidai kuwa kampeni hiyo imelenga kupinga vitendo vya ukeketaji ambavyo vinavyotarajiwa kutekelezwa mwakani 2018, kwani ndio mwaka mahususi kwa kukeketa hususani kwa makabila yanayotokea mkoani mara ambayo yameshamili katika kata hiyo.

Aliendelea kusema kuwa watekelezaji wakuu wa mambo haya ni watu tunaoishi nao katika jamii zetu na kesi zake zinakuwa ngumu kusikilizwa kutokana kwamba watekelezaji wa hayo ni baba, mama au shangazi hivyo inaleta ugumu katika kutoa ushahidi na mtoto anaogopa kwa kuwa anajua mzazi wake au ndugu yake atafungwa kwa sababu yake.

“Wanaharakati wengi wamekuwa wakisubiri zoezi la kukeketa lianze ndipo waanze kuwakamata wahusika wakiwa tayari wameshakeketa, lakini kwetu sisi tumeona tuzuie kabla watoto hawa hawajafanyiwa ukeketaji ili kuweza kuwakomboa juu ya mila na tamaduni mbaya kama hizi” alisema bishagazi

“Kampeni hii itakuwa ni endelevu lakini pia tutajaribu kuwa karibu na wananchi ili waweze kutupa taarifa mbalimbali kuhusu wakeketaji na tutakaa nao chini tutajaribu kuwapa elimu juu ya madhara ya ukeketaji ili waachane na mambo hayo ya kizamani na mila potofu ya kukeketa na waweze kuwa watu wema katika jamii”. Alisema Mkurugenzi huyo

Lakini pia katika maeneo mengi hususani maeneo ya kazi, vyuoni, mashuleni maeneo ya biashara wananchi wanalazimishwa sana kutoa rushwa ya ngono ili waweze kupata huduma stahiki wanayohitaji, ndio maana sauti jamii kipunguni imeamua kuanzisha kampeni hii ya kupinga rushwa ya ngono katika jamii zetu.

Sauti jamii kipunguni kwa kushirikiana na Women Fund tutawezeza kutoa elimu kwa wananchi na kuwawajibisha waajili, madaktari, walimu na watu wote walio katika sekta za Umma na binafsi ili waweze kupinga na kutoa taarifa kwa vyombo husika endapo wataombwa rushwa ya ngono watu hao.

                          ANGALIA VIDEO HII KUJUA KILICHOENDELA ZAIDI...
                        
JULIANA SHOZA ATOA ONYO HILI KWA WASANII WA BONGO

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza amesema wizara yake haitasita kumchukulia hatua msanii yeyote ataekaidi agizo la kuvaa mavazi yenye staha.
 Picha inayohusiana
Naibu Waziri huyo ameyasema hayo katika uzinduzi wa Tamasha la Tanzania Tukuza Utalii Festival lenye lengo la kukuza utalii lililoandaliwa na Shirikisho la Waimbaji wa Nyimbo za Injili chini.

“Wasanii wote ambao wataendelea kukaidi agizo la mheshimiwa Rais la kutokuvaa mavazi ya staha Wizara yangu haitawavumilia tutachukua hatua kwa yeyote bila kujali nafasi au umaarufu wake, kabla dhoruba haijawakumba wabadilike, kwenye kupiga rungu siangalii mtu usoni.,”amesema Naibu Waziri Shonza.

Siku chache zilizopita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli wakati akihutubia Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi CCM alitoa tamko la kuwataka wasanii kuvaa mavazi ya heshima katika video za nyimbo zao.

TRA WAJA NA HILI KWA ASKOFU KAKOBE

Kufuatia Kauli ya Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakary Kakobe kudai kuwa ana pesa nyingi kuliko serikali, mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamepanga kumchunguza kiongozi huyo wa dini.
Tokeo la picha la ASKOFU KAKOBEHayo yamesemwa leo na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo amesema;

“Tupokea kauli ya Askofu Kakobe kwa unyenyekevu mkubwa sana kwa kuwa wao wanapenda watu wenye pesa nyingi ili waweze kupata haki yao

“Kama mtu ana hela kuliko serikali, kama ambavyo tunajua serikali yetu inatoa huduma inanunua ndege, imejenga standard gauge, inajenga barabara, inatoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia madawa hospitalini, inalipa na kutoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi. Lakini Serikali hiyo tunaambiwa inazidiwa hela na Askofu Kakobe basi ni jambo jema.

“Tunawafahamu matajiri wanalipa kodi, baada ya kauli ya Askofu Kakobe tukaanza kupitia kumbukumbu zetu ili kuona namna Askofu Kakobe anavyolipa Kodi. Kakobe aliyesema anaizidi Serikali kwa pesa hakuna kumbukumbu za ulipaji kodi wake. Sisi Wataalamu wa mambo ya kodi tutafahamu tu kama utajiri wake anaousema unatokana na sadaka tu au kuna shughuli nyingine za kiuchumi anafanya”

“Tunaelewa kwa mujibu wa sheria sadaka haitozwi kodi, ila tunafahamu taasisi za dini huwa zina shughuli nyingine za kiuchumi, huenda Askofu Kakobe na yeye akawa na shughuli nyingine zinampatia hela mpaka akawa na pesa nyingi kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini pia kama kweli ni sadaka pekee inayomfanya Askofu Kakobe awe na pesa nyingi kuliko Serikali ni jambo la kushtua kidogo. Basi hizo sadaka ni nyingi kweli kweli na watoa sadaka watakuwa matajiri kweli kweli,” alisema Kichere.

Aidha TRA wamemtaka Askofu Kakobe kutoa ushirikiano ili wajiridhishe juu ya utajiri wake na ulipaji kodi wake.

MRISHO GAMBO AMTOLE UVIVU ASKOFU KAKOBE

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa kuna haja kubwa ya kuyafanyia uchanguzi makanisa ili kuweza kujua makanisa halisi ili kuweza kutofatisha na mawakala wa shetani.

Ameyasema hayo jijini Arusha ambapo amesema kuwa baadhi ya makanisa yamekuwa yakiwapotosha wananchi kwa kuwajaza imani isiyokuwa ya kibinadamu.

Amesema kuwa historia ya mchungaji Kakobe inatia mashaka kwani amebeba vyeo vyote vya kanisa hata anaposafiri huwawekea waumini wake ‘Cassete’ ili wamsikilize akiwa safarini.

“Kuna watu wengine ni mawakala wa shetani, hivyo kuna kila haja ya kuanza kufanya uchambuzi wa makanisa haya ambayo yamekuwa yakipotosha Watanzania, unaofanywa na anayejiita Askofu Kakobe ni umburula,”amesema Gambo

Hata hivyo, ameongeza kuwa taasisi ya dini ina utaratibu wake inaheshimika, ina mfumo wake na inathaminika katika jamii.

==>Msikilize hapo chini

ANGALIA PICHA ZA LISSU AKIWA AMEANZA KUKAA MWENYEWE

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amekaa mwenyewe pasipo msaada wa madaktari katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya, anakotibiwa baada ya kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake, Area D, Dodoma huku hali yake ikizidi kuimarika kila kukicha.

Desemba 26, mbunge huyo alisimama kwa mara ya kwanza na kuanza rasmi kufanya mazoezi ya viungo katika Hospitali hiyo kwa msaada wa madaktari. Lissu anaendelea na mazoezi madogo ya kuimarisha misuli ya miguuni ili aweze kutembea.

Akielezea hali yake, Mhe. Tundu Lissu amesema kwa sasa anauwezo wa kukaa bila kuegemea kwenye kitu chochote, hali ambayo awali alikuwa anashindwa kufanya hivyo.

“Ninawashukuru kwa sala na maombi yenu. Sasa ninaweza kukaa bila ya kuegemea kitu.“ameandika Mhe. Lissu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwanasheria mkuu huyo wa Chadema, ambaye alishambuliwa kwa risasi akiwa ndani ya gari mara baada ya kufika nje ya makazi yake mjini Dodoma Septemba 7, hivi karibuni alisema bado ana risasi moja mwilini mwake ambayo haijatolewa.

Friday, December 29, 2017

SAUTI JAMII KIPUNGUNI YAENDESHA KAMPENI KABAMBE YA KUPINGA UKEKETAJI KATIKA KATA HIYO

Watoto kutoka mitaa mbalimbali ya kata ya Kipunguni wakilifuata gari la matangazo la Sauti Jamii Kipunguni na kuzipokea kwa furaha huduma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ikiwa ni kugawa vipeperushi na kutoa elimu bure, mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya Akeketwi mtu mwaka 2018.
Mchungaji wa kanisa la Sinai Pentecostal Ndugu. Imani Juma Feruzi akibandika karatasi yenye ujumbe(posters) katika pikipiki mapema jana, katika uzinduzi wa kampeni ya akeketwi mtu mwaka 2018 iliyoandaliwa na Sauti Jamii Kipunguni ili kupinga vitendo vya Ukeketaji na Rushwa ya ngono.

Mwanaharakati wa Sauti Jamii Kipunguni Bi. Tausi Msangi akibandika karatasi yenye ujumbe(posters) katika moja ya duka la dawa linalopatikana katika kata ya kipunguni, mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya Akeketwi mtu mwaka 2018.
Wanaharakati wa Sauti Jamii Kipunguni wakiwa na watoto mbalimbali wa kata ya hiyo wakiwa wameshika mabango yenye jumbe tofauti tofauti kuashiria kuchoshwa na vitendo vya ukeketaji vilivyoshamili katika kata hiyo, mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya Akeketwi mtu mwaka 2018.

Mkurugenzi wa Sauti Jamii Kipunguni Bw. Selemani Bishagazi akigawa vipeperushi kwa wakazi mbalimbali wa kata ya Kipunguni eneo la Machimbo, katika uzinduzi wa kampeni ya akeketwi mtu mwaka 2018 mapema jana jijini Dar es salaam.
Wanaharakati wa kata ya kipunguni wakicheza kwa pamoja na watoto wa kata hiyo mara baada ya kuwapa elimu juu ya kupinga ukeketaji na rushwa ya ngono mapema jana jijini Dar es salaam.

Wanaharakati wa kata ya Kipunguni wakiwa katika picha ya pamoja mapema jana jijini Dar es salaam.

Na Vicent Macha

Kituo cha Sauti jamii Kipunguni jana tarehe 29 mwezi desemba kimezindua kampeni mahususi ya kutoa elimu mtaa kwa mtaa, iliyofuatiwa na zoezi la kugawa vipeperushi pamoja na kubandika karatasi zenye jumbe mbalimbali katika kata hiyo.

Akiongoza kampeni hiyo Mkurugenzi wa Sauti jamii Kipunguni Bw. Selemani Bishagazi alisema kuwa lengo kuu la kampeni hiyo kuangazia sehemu kuu mbili ambazo ni kupinga ukeketaji katika kata hiyo lakini pia rushwa ya ngono katika jamii ya kitanzania.

Aidha Bw. Bishagazi alidai kuwa kampeni hiyo imelenga kupinga vitendo vya ukeketaji ambavyo vinavyotarajiwa kutekelezwa mwakani 2018, kwani ndio mwaka mahususi kwa kukeketa hususani kwa makabila yanayotokea mkoani mara ambayo yameshamili katika kata hiyo.

Aliendelea kusema kuwa watekelezaji wakuu wa mambo haya ni watu tunaoishi nao katika jamii zetu na kesi zake zinakuwa ngumu kusikilizwa kutokana kwamba watekelezaji wa hayo ni baba, mama au shangazi hivyo inaleta ugumu katika kutoa ushahidi na mtoto anaogopa kwa kuwa anajua mzazi wake au ndugu yake atafungwa kwa sababu yake.

“Wanaharakati wengi wamekuwa wakisubiri zoezi la kukeketa lianze ndipo waanze kuwakamata wahusika wakiwa tayari wameshakeketa, lakini kwetu sisi tumeona tuzuie kabla watoto hawa hawajafanyiwa ukeketaji ili kuweza kuwakomboa juu ya mila na tamaduni mbaya kama hizi” alisema bishagazi

“Kampeni hii itakuwa ni endelevu lakini pia tutajaribu kuwa karibu na wananchi ili waweze kutupa taarifa mbalimbali kuhusu wakeketaji na tutakaa nao chini tutajaribu kuwapa elimu juu ya madhara ya ukeketaji ili waachane na mambo hayo ya kizamani na mila potofu ya kukeketa na waweze kuwa watu wema katika jamii”. Alisema Mkurugenzi huyo

Lakini pia katika maeneo mengi hususani maeneo ya kazi, vyuoni, mashuleni maeneo ya biashara wananchi wanalazimishwa sana kutoa rushwa ya ngono ili waweze kupata huduma stahiki wanayohitaji, ndio maana sauti jamii kipunguni imeamua kuanzisha kampeni hii ya kupinga rushwa ya ngono katika jamii zetu.

Sauti jamii kipunguni kwa kushirikiana na Women Fund tutawezeza kutoa elimu kwa wananchi na kuwawajibisha waajili, madaktari, walimu na watu wote walio katika sekta za Umma na binafsi ili waweze kupinga na kutoa taarifa kwa vyombo husika endapo wataombwa rushwa ya ngono watu hao.

                          ANGALIA VIDEO HII KUJUA KILICHOENDELA ZAIDI...

MHE MWANJELWA ATOA SIKU MOJA KWA WAFANYABIASHARA WALIOFUNGA MAGHALA YA MBOLEA LA SIVYO KUNYANG'ANYWA LESENI

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akikagua mbegu zilizohifadhiwa ghalani kabla ya kuanza kusambazwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge (Kulia) na Meneja uzalishaji Wakala wa Mbegu Ndg Charles Levi (Kushoto). Picha Zote Na Mathias Canal 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo baada ya kukagua baadhi ya mashine za mbegu alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua namna mbegu za mazao mbalimbali zilivyohifadhiwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. 

Na Mathias Canal, Morogoro

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo Disemba 29, 2017 amewaagiza wafanyabiashara wa mbolea kote nchini walioweka mgomo wa kupeleka mbolea kwa wakulima kufikia 30 Disemba 2017 wawe wamefungua maghala yao kwa ajili ya kuwauzia mbolea wakulima.

Alisema endapo wafanyabiashara hao wasipofanya hivyo serikali itawanyang'anya leseni zao haraka iwezekanavyo ili kuruhusu wafanyabiashara wenye uwezo wa kufanya jukumu hilo pasina kuwaumiza wakulima kutokana na bei ghali ya mbolea.

Mhe Mwanjelwa ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) Mara Baada ya kubaini kuwa kuna wafanyabiashara ambao wameanza kufunga maghala kwa madai ya kupanda kwa mbolea katika soko la Dunia.

Alisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na kuijaribu serikali kwani malalamiko yao ya kupanda kwa bei katika soko la Dunia hayana tija kwani mbolea zote zilipo nchini tayari wakishanunua kipindi soko likiwa kwenye unafuu mkubwa.

Alisema kuwa serikali ilitoa bei elekezi katika mbolea ya kukuzia na kupandia ikifahamu fikra kuwa kupitia gharama hiyo wakulima watanufaika lakini pia wafanyabiashara watanufaika kutokana na faida wanayoipata lakini wameamua kubadili utaratibu wa kutaka kupata faida kubwa zaidi pasina kujali wakulima wataumizwa na bei hiyo kwa kiasi gani.

Mhe Mwanjelwa ameitaka kampuni ya Premium ambayo ni moja ya kampuni zilizogoma kufungua maghala na kupeleka mbolea kwa wakulima kwa bei elekezi iliyotolewa na serikali.

Alisema kuwa wafanyabiashara hao kwa makusudi wameamua kufifisha juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ya kuwakomboa wakulima kupitia gharama nafuu ya mbolea hivyo kufikia kesho wasipofungua maghala hayo watanyang'anywa leseni zao ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa sheria.

Wateja wa Tigo Pekee Wanafurahia Bonasi za Bure kwa Bando Zote

                                        Tokeo la picha la tigo logo
Tofauti na taarifa zilizochapishwa zinadozai kuwa Tigo ndio mtandao wenye gharama kubwa zaidi, Tigo ingependa kuwataarifu kuwa wateja wetu wanafurahia mojawapo ya gharama nafuu zaidi nchini.

Bando zetu zinaanzia TZS 500; hakika wateja wa Tigo wanaonunua bando ya sauti ya TZS 500 kupitia menu yetu mpya ya 147*00 wanapata dakika 16. Pamoja na hili, wateja wa Tigo wanaonunua bando hii wanapokea bonasi ya dakika tano (5) BURE kila mara wanaponunua bando hii kupitia promosheni ya TUMEKUSOMA ambayo inawapa jumla ya dakika 21. Kwa hiyo kwa bando la TZS 500, bei zinaweza kufikia TZS 17.2 kwa dakika bila kujumuisha kodi.

Bando ya TZS 1000 inayonunuliwa kupitia *147*00# inawapa wateja wetu dakika 55, ambapo pia wanapokea bonasi ya dakika 30 BURE kupitia promosheni ya TUMEKUSOMA. Hii inawapa jumla ya dakika 85; kwa hiyo bei inaweza kufikia TZS 8.5 kwa dakika bila kujumuisha kodi.

Tigo inajulikana kwa promosheni kabambe na ubunifu wa ofa. Tigo pia imejijengea jina kama mtandao unaowaelewa zaidi wateja wake na kuwapa bidhaa zinazoendana na mahitaji ya soko.

Wateja wa Tigo ndio watumiaji wa simu pekee wanaopokea bonasi za bure kwa kila bando wanayonunua, hivyo kuhakikisha kuwa wateja wa Tigo wanafurahia huduma bora zaidi kwa viwango bora na nafuu nchini.

Kupitia huduma zake za kipekee za sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi ya juu ya 4G na huduma za kifedha kupitia simu za mikononi, Tigo inaongoza kwa ubunifu wa kidigitali ikiwemo;
  • Tigo Halichachi ndio bando ya kwanza iliyowezesha wateja wa simu nchini kutumia bando zao za simu bila muda wa ukomo wa matumizi.
  • Kuwa kampuni ya kwanza ya simu kuzindua simu za Smartphone zenye lugha ya Kiswahili
  • Kuwa kampuni ya kwanza ya simu kuzindua Facebook ya bure kwa lugha ya Kiswahili
  • Kampuni ya kwanza ya simu kuzindua huduma za fedha kupita smart apps
  • Huduma ya kwanza yenye uwezo wa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya nchi husika Afrika Mashariki iliyowezesha wateja kufanya miamala ya uhakika ya fedha kupitia simu za mkononi kwenda nje ya nchi.     

Tigo pia inajivunia mtandao mpana, wa uhakika zaidi wa 4G nchini, uliosambaa katika miji 24 Tanzania, hivyo kuwawezesha wateja kufurahia maisha ya kidigitali.

TAMKO LA BASHE KWA POLISI WA KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM

Wakati Jeshi la Polisi Tanzania kupitia kanda maalum ya Dar es salaam likitangaza kuwa lazima litamhoji Askofu na kiongozi wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Zachary Kakobe kwa madai ya kutoa maneno ya kashfa kwenye mahubiri yake, wapo Wanasiasa walioguswa na taarifa hii na mmoja wapo ni Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe.

Kupitia akaunti ya twitter Mbunge Hussein Bashe ameandika ;"Kesho tutazitaka Taasisi za Dini zihamasishe amani,Maendeleo, zipongeze ni muhimu kukubali kukosolewa, Serikali haitakiwi kufanya hivi kama hazivunji sheria.

"Taasisi za Dini zina haki ya kutoa maoni yao juu ya siasa,Uchumi na maswala yote ya kijamii, viongozi wa Dini wana nafasi yao"

KESI YA MALINZI NA WENZAKE YAPIGWA KALENDA MWAKA MPYA KULA WAKIWA JELA

Kesi  ya  kutakatisha Dola za Marekani 375,418 inayomkabili aliyekuwa Rais wa shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake, imepigwa kalenda hadi Januari 11, 2018 baada ya upande wa Jamhuri kudai bado haujakamilika.

Hata hivyo,  upande wa utetezi uliiomba  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  Dar es Salaam, kuuamuru upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo.

Kesi hiyo ilitajwa jana na  Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Leonard Swai, alidai kuwa  upelelezi bado haujakamilika, hivyo akaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko, alidai kuwa kesi hiyo ni ya muda mrefu na kila siku wanaambiwa jalada bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Hakimu Mashauri alisema mahakama hiyo inafanya kazi ya kutafsiri sheria na kama itafanya vinginevyo itakuwa nje ya sheria.

Alisema kesi hiyo itatajwa Januari 11, 2018 na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga ambao wanakabiliwa na mashtaka 28, ikiwamo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.