Miongoni mwa
haki muhimu za binadamu ya kwanza ni kuishi na ya pili ni kupokea na kutoa
taarifa katika jamii kwa usahihi.
Waandishi wa habari wakijadiliana kwa pamoja na wadau kutoka Asasi za kiraia mapaema jana jijini Dar es salaam. |
Hayo
yamesemwa mapema jana Kunduchi Beach na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sharia na Haki za Binadamu Bi. Anna Henga katika semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo ambayo iliwakutanisha
waandishi wa habari na watu wa asasi za kiraia.
Anna Henga
alisema lengo kuu la semina hiyo ni kuwakutanisha wanahabari na wadau mbalimbali kutoka katika asasi za kiraia(Azaki) kujaribu kuwaweka pamoja na kuona kwa jinsi gani wanaweza kufanya kazi pamoja licha
ya kuwa wanawekewa sharia ngumu zinazowabana.
Aliendelea
kusema kuwa haya makundi mawili yanategemeana kwa kuwa wanahabari wanategemea
kupata habari katika azaki na wana azaki wantegemea wanahabari ili kufikisha ujumbe
wao kwa jamii husika.
Lakini pia
kuunganisha nguvu za pamoja endapo mmoja wao atapata tatizo katika kazi yake
basi kundi linguine liweze kutoa ushirikaiano wa kuona wata msaidia vipi
mwanaharakati mwenzao, kwani kwa sasa kuna sharia ngumu zinazoyabana makundi
yote mawili.
Bw. Fungis Masawe kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu akitoa elimu ya sheria kwa waandishi wa habari pamoja na wana azaki mapema jana Kundichi Beach jijini Dar es salaam. |
Hivyo wananchi
wanatakiwa kuwa macho sana ili wasije wakaingia kwenye ujinai kwani mtu
atakeyetenda kosa hili atahesabiwa ametenda kosa la jinai, na wananchi
wanatakiwa kupewa elimu ya kutosha katika matumizi ya hii mitandao kama
facebook, watsaap nk.
Washiriki wa semina ya wanahabari pamoja na wadau kutoka asasi za kiraia iliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wakiwa katika picha ya pamoja mapema jana Kunduchi jijini Dar es salaam. |
Na pia
alisema kuwa sheria hii inambana mtoa taarifa lakini haikutoa muongozo kwamba
nini afanye mtu huyu endapo mtu Yule ambaye ni chanzo cha habari akigoma kutoa
taarifa wakati mtoa taarifa atakapohitaji kujiridhisha kwa chanzo chake.
Bwana fungis
aliendelea kusema kuwa kuna sheria ya takwimu ambayo nayo inakataza kutoa
takwimu hata kama ni za kweli mpaka utakapopewa idhini na idara husika la sivyo
unahesabiwa unakosa la jinai kwa kutoa takwimu bila ruhusa hali inayofanya
kukosekana kwa ukweli wa vitu vingi katika nchi yetu.
BONYEZA HAPA KUJUA MENGI ZAIDI KUHUSU SHERIA YA MITANDAO..
No comments:
Post a Comment